Mtoto Aliyefariki Miaka Minne Iliyopita Na Kuzikwa Akutwa Akiwa Hai, Kaburi Lafukuliwa


Na Joel Maduka Geita

Mtoto mwenye miaka 11 mkazi wa kijiji Cha Ngemo kata Ngemo wilaya ya Mbogwe Mkoani Geita amezua taaruki kwa kuonekana hai tena baada ya kufariki miaka 4 iliyopita

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Geita kamishana msaidiizi Henry Mwaibambe amesema mtoto huyo aliyejulikana kwa jina Leonard morisha alifariki tarehe 27 mwezi wa 6 mwaka 2017 na kuzikwa kijijini kwao Ngemo ,na kushangaza watu kwa kuonekana tena katika kijiji cha Segesa wilayani Kahama october 2020 na wazazi wake wakampata na kumtambua Tar 12 Desemba mwaka huu.

Katika maelezo yake Acp Mwaibambe amesema mama wa mtoto huyo alifahamika Tereza Lusolela miaka (48) alithibitisha kuwa kuwa huyo Ni mwanaye na baada ya jeshi la polisi kufukua kaburi hakukutwa sanduku Wala vipande vya kanga ambavyo mama amedai walimzikia mwane miaka 4 iliyopita

Sambamba na Hilo ACP Henry Mwaibambe ameziomba hospitali kubwa kumsaidia kimatibabu mtoto huyo, kwa Sasa haongei baada ya kuonekana hai huku Ulimi wake ukiwa Umekatwa.



from MPEKUZI

Comments