Watu wawili wamefariki Dunia katika ajali iliyohusisha Malori mawili iliyotokea eneo la Mkambarani barabara ya Morogoro – Dar es alam nje kidogo ya Manispaa ya Morogoro .
Katika Malori hayo, moja lilibeba shehena ya Saruji likiwa linatokea Dar es Salaam kuelekea Morogoro lenye namba za usajili T 389 DXF likiwa na Tela namba T452BCR na jingine lilikua linatokea Morogoro kuelekea Dar es Salaam lenye namba za usajili T 708CCT tela namba T 927 CNF yaligongana uso kwa uso na kusababisha vifo vya watu wawili .
Ajali hiyo ambayo imetokea majira ya saa 11 Alfajiri ya Disemba 16, 2021 ilisababisha foleni kwa watumiaji wa barabara hiyo kwa zaidi ya saa tatu.
Akizungumza kwa njia ya simu kamanda wa Polisi mkoa Morogoro, Fortunatus Musilimu amekiri kutokea kwa ajali hiyo huku Katibu wa Hospitali ya Rufaa mkoa Morogoro, Scolastika Solomoni amekiri kupokea miili ya watu wawili ambao wote ni wanaume ambao wamefariki katika ajali hiyo na kwamba hadi sasa bado miili hiyo haijatambulika.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment