Baada ya sintofahamu nyingi kuhusu kuadimika kwa toleo la modeli mpya ya Infinix HOT 11 sasa rasmi zimeanza kupatika tena sokoni. Infinix HOT 11 ilizinduliwa rasmi 14/12/2021 kwa ushirika wa Infinix na Tigo na kuwa adimu kwa muda wa siku kadhaa baada ya uzinduzi sasa modeli hiyo inayosifika kwa kuwa na camera kali zaidi imeanza kupatikana tena sokoni.
Infinix HOT 11 imebebeshwa features ambazo tumezoea kuziona katika matoleo makuu ya kampuni hiyo kama Infinix NOTE series na baadhi ya features hizo ni battery la mAh6000, kamera Megapixel 50, Memory ya GB128 kwa Ram ya GB4 na refreshi rate ya 90Hz kuwekwa zote kwa pamoja kwenye toleo hili la HOT 11 na kuifanya HOT 11 kuwa na hadhi ya juu zaidi kuzidi matoleo ya awali ya series za HOT.
Naomba nikurudishe nyuma kidogo ndugu msomaji “Infinix HOT series ni toleo lenye kulenga vijana wote wa Kitanzania ambao kupitia tech wamekuwa wakijifunza mengi kuhusu namna dunia inavyoenda kwa sasa na hata kuifanya simu kama sehemu ya ajira na kwasasabu hizo basi Infinix ndio maana tumeona ni vyema kuifanya HOT 11 kuwa na features mahiri zaidi ambazo tumezoea kuziona kwenye series nyengine za matoleo ya Infinix kama vile NOTE n.k”, alisema Afisa Uhusiano Infinix wakati wa Uzinduzi huo.
“Infinix HOT 11 ni simu ya kijana wa kisasa kuanzia namna inavyoonekana, inavyoweza kuperform vitu mbalimbali kama kuchezesha games, kupiga picha ya qualiti ya juu, kuhifadhi kumbukumbu nyingi na kuangalia movies katika kioo cha wigo wa inch 6.82 kwa battery ya mAh6000 lenye kukufanya ujimini zaidi kuwa hauwezi ishiwa chaji kirahisi alimaliza Aisha Karupa”.
Katika msimu huu wa sikukuu za Kristmass na Mwaka mpya Infinix kuwazawadi wateja wa Infinix HOT 11 zawadi mbalimbali kama TV ya inch 55, fridge n.k tembelea maduka yao sasa usipitwe na ofa hizi.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment