Disco Toto Marufuku Mwaka Mpya Mkoani Tabora


Na Lucas Raphael,Tabora
Jeshi la Polisi Mkoa wa Tabora limepinga marufuka disco toto ,uchomaji wa moto matairi kuweka miti barabarani na kupikaji wa mafataki katika  kusheherekea mwaka mpya wa 2022

Kamanda Wa Polisi mkoani hapa, Richard Abwao alitoa kauli hiyo alipolikuwa akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake alisema kila mtu kuzingatia na kufuata maelezo ya jeshi hilo kuacha kufanya vitendo hivyo ambavyo ni hatari kwa watu wengine hasa wale wenye matatizo ya moyo na matatizo ya Afya.

Alisema jambo nzuri sana kufuata sheria bila shuruti kuzingati hasa kipindi hiki cha  kupambano na uviko 19 na kusisitiza wananchi wanatakiwa kuzifuata  sheria hasa katika kipindi hicho cha mwisho wa mwaka na kukaribisha mwaka mpya .

Alisema kwamba wenye magari kutoendesha magari wakiwa wamelewa na wananchi  kuzingatia sheria za usalama barabarani ,kuweka ulinzi katika makazi yao na wale watakaonde kwenye ibada ya mkesha  wahakikishe wamemuacha mtu nyumbani na kuweka ulinzi kwa watoto  

Aidha kamanda huyo amewataka waendesha  bodaboda kuchukua taadhari nyakati za usiku na kutokubali kukodiwa na watu wasiwafahamu kwenda umbali mrefu .

Wakati huyo huo jeshi hilo  linashikilia Edson Bileba (33)  mkazi wa ndala mkoani Tabora alikamatwa akiwa na noti Bandia za kimarekani (Dola )17 zenye thamni ya dola 4600 sawa na shilingi milioni 10,607,600.

Akizungumza na waandishi wa habari jana kamanda wa Polisi mkoani hapa Richard Abwao alisema kwamba tukio hilo lilitokea mnamo desemba 10 mwaka jana katika Tawi la benki ya NMB mihayo kata ya kanyeneye wilaya ya Tabora na mkoa wa Tabora

Alisema kwamba mtuhumiwa huyo alikwenda benki kwa lengo la kuta kuzibalidilisha fedha hizondipo walipobaini bna kasha kumkamata kabla ya kutimiza azma yake .

Alisema kwamba jeshi hilo linaendelea kumuhoji mtuhumiwa huyo na baada kukamilika kwamupelelezi hatafikiwashwa mbele ya sheria kujibu mashitaka yanayomkabili.


from MPEKUZI

Comments