Mahakama imekubali kupokea nyaraka ambazo upande wa utetezi katika kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake watatu wanataka kuzitumia kuthibitisha askari Ricardo Msemwa aliyedai kumpokea mshtakiwa wa pili katika Kituo Kikuu cha Polisi, Dar es Salaam hakuwa akifanya kazi kituoni hapo.
Haya yamekuja baada ya mahakama kutupilia mbali mapingamizi matatu yaliyowasilishwa na upande wa mashtaka kuhusu nyaraka mbalimbali na barua kwa hakimu mkazi Kisutu kutohusika na shauri hilo dogo lililopo mahakamani hapo.
Wiki iliyopita,Msemwa alisema Agosti 2020 alikuwa kazini Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam na ndiye aliyempokea Mohamedi Ling’wenya na wenzake na kuingiza taarifa zao katika kitabu cha kumbukumbu za mahabusu.
Akitoa uamuzi huo leo Jumanne Novemba 30, 2021 Jaji Joachim Tiganga amesema kuwa Mahakama imeona ivipokee vielelezo vyote ambavyo ni barua kwenda kwa hakimu Mkazi Kisutu, dispatch, hati ya mashtaka na Mwenendo wa shauri lililokuwa Kisutu.
Jaji : Mara baada ya mawakili kutoa hoja zao Mahakama ilienda mapumziko lakini pia ikasema inaweza kuwaita mawakili ili kutoa maelekezo sasa inatoa amri ifuatayo .
Jaji :Jana shahidi wakati akitoa ushahidi aliomba kutoa vilelezo lakini upande wa mashtaka umezipinga kwanza ukisema nakala ya hati ya mashtaka ni nakala kivuli, shahidi hajaonesha kuwa anastahili kutoa kielelezo
Jaji : Mahakama imezingatia hoja zote na kwamba vielelezo hivi vinalenga kutolewa kwenye kesi ndogo na baada ya kuzingatia upokeaji vielelezo huzingatia vigezo vya awali na kwa kuzingatia. Kuwa pande zote zinabaki na haki ya kuchunguza udhaifu wake basi Mahakama umeona ivipokee vielelezo vyote ambavyo. Ni barua kwenda kwa hakimu Mkazi Kisutu, dispatch, hati ya mashtaka na Mwenendo wa shauri lililokuwa Kisutu.
Jaji : Mahakama Kama ilivyosema inapokea vielelezo hivyo kwa nafasi ya kujipa muda wa kuvichunguza. Hivyo naomba vielelezo hivyo shahidi akabidhiwe avisome kimoja kimoja
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment