Ndugu Wananchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imekamilisha zoezi la uchaguzi wa wanafunzi wa kujiunga na Kidato cha Kwanza mwaka 2022.
Zoezi hilo limehusisha jumla ya wanafunzi 907,802 wakiwemo Wasichana 467,967 na Wavulana 439,835 ambao ni sawa na asilimia 81.97 ya wanafunzi waliofanya Mtihani wa Kuhitimu Elimu ya Msingi mwaka 2021. Kati ya waliofaulu na kupangiwa kujiunga na kidato cha kwanza wamo Wanafunzi wenye mahitaji maalum 2,673 sawa na asilimia 0.29 ambao kati yao wavulana ni 1,471 na wasichana 1,202.
Kwa mwaka 2022 kumekuwa na ongezeko la wanafunzi 73,932 sawa na asilimia 8.87 ya wanafunzi waliofaulu ukilinganisha na mwaka, 2020 ambapo jumla ya wanafunzi 833,872 walifaulu na kupata sifa ya kujiunga na masomo ya Kidato cha Kwanza.
_______
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment