Bodi Wa Nyama Nchini Yapiga Marufuku Matumizi Ya Dawa Za Kuulia Nzi Na Wadudu Wengine Kupulizwa Kwenye Mabucha


 Na Lucas Raphael,Tabora
Bodi wa nyama nchini imepiga marufuku matumizi ya dawa za kuulia nzi na wadudu wengine kupulizwa kwenye mabucha  wakati nyama ikiwemo ndani  ,jambo ambalo linalohatarisha maisha na afya za wanunuzi wa kitoweo hicho.

Alisema dawa hizo ni sumu hatari  zinafanya kazi taratibu ndani ya mwilini mwa binadamu na mwisho wa siku zinasababisha maradhi mbalimbali yakiwemo kansa .

Rai hiyo ilitolewa jana na Afisa wa Bodi ya Nyama kanda ya kanda ya Magaharibi ,Joseph kulwa wakati akitoa elimu kwa wadau wa nyama katika kata ya Nata wilaya ya Nzega mkoani Tabora.

Alisema kuwa baadhi ya mwenye  mabucha wamekuwa wakitumia dawa za kuulia wadudu kuwauwa nzi maarufu (Rungu )wakati nyama ikiwemo kwenye bucha kitendo ambacho ni hatari sana kwa  walaji wa nyama .

Alisema kwamba bucha nyingi mazingira sio rafiki ni machafu hivyo nzi wanavutiwa nayo ni muhimu kwa wamiliki wa mabucha hayo weka mazingira ya usafi ilikuepukana na jambo hilo.

Alisema kwamba nikosa la jina kupulizia dawa ya kuulia wadudu kwenye eneo ambalo lina vyakula vya binadamu nani hatari hata kwa muuza nyama mwenyewe.

“Tumeamua kutoa tahadhari hiyo mara kwa mara ili kuacha kabisa kutumia dawa za kuuliza wadudu kwa ajili ya kuulia nzi wakati bucha ina nyama tutakuchua hatua kali za kisheria ili kukomesha vitendo hivyo”alisema Kulwa .

Naye Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa nyama  kata ya Nata, Said Salum alisema kwamba wataitumia elimu hiyo kama darasa muhimu la  kuweza kupunguza mapungufu ambayo walikuwa nayo kwenye mabucha yao .
Alisema elimu waliyoipata ni elimu ambayo wengi wao walikuwa hawana hivyo ni muhimu kuifanyia kazi kwenye tasni hiyo.

Hata hivyo wafugaji wa mifugo wilayani nzega wametakiwa kuhakikisha wanasajili  bucha zao ili waweze kufanya biashara ya kuuza nyama na wale ambao hawataweza kufanya usajiliwa hawataweza kufanya biashara hiyo tena .


from MPEKUZI

Comments