Wanandoa wauawa kwa mapanga mkoani Njombe


ANES Haule (45) na mume wake Menluph Ngailo (45) wameuawa kwa kukatwakatwa mapanga wakiwa wamelala nyumbani kwao huko kijiji cha Itacha Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe, Hamis Issah, amesema tukio hilo limetokea Oktoba 19,2021 majira ya saa mbili usiku.

"Hawa wanandoa wakiwa nyumbani kwao walivamiwa na watu wakiwa na silaha zenye ncha kali na waliwasababishia majeraha kichwani,shingoni,mashavuni,begani na majeraha haya ndio yamepelekea wanandoa hao kufariki," amesema Kamanda.

Kamanda amesema kuwa jeshi la polisi liliingia kazini na kubaini waliohusika na tukio hilo ambao ni ndugu wawili na kuwakamata.

"Baada ya vielelezo fulani vinavyohusiana na uchunguzi kuonekana kuwa wamehusika ni wanandugu wakike na wa kiume ambao ni Nuru Ngailo na wa pili ni Evarinjista Ngailo huyu ni dada wa marehemu hawa walikua wanamtuhumu ndugu yao kuwa ni mshirikina kwa sababu wao walikua wakiishi katika mazingira ya kuumwa umwa wakasema wanarogwa na huyo kaka yao wakishirikiana na mke wake"amesema.




from MPEKUZI

Comments