Na Mwandishi wetu, Babati
TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoani Manyara imechunguza miradi 19 ya thamani ya shilingi bilioni 5.5 ili kujiridhisha iwapo kuna matumizi sahihi ya fedha hizo.
Mkuu wa TAKUKURU Mkoani Manyara, Holle Joseph Makungu ameyasema hayo wakati akisoma taarifa ya utendaji kazi kwa kipindi cha miezi mitatu ya Julai hadi Septemba kwa waandishi wa habari mjini Babati.
Makungu amesema wametembelea miradi mbalimbali ikiwemo ya ujenzi wa madarasa, hospitali, vituo vya rasilimali vya kilimo, barabara, madaraja na mabweni ya shule ya sekondari.
Amesema katika kipindi hicho cha miezi mitatu wamepokea malalamiko 85 ya mashtaka mbalimbali ambayo 65 ilikuwa ya rushwa na 20 hayakuhusianan na matukio ya rushwa.
Amesema malalamiko hayo 65 wameyafikisha mahakamani na hayo 20 wamewaelekeza walalamikaji ipasavyo.
Amesema wamepanga kuanza utekeleza wa mpango wa kitaifa wa kutoa elimu kwa vijana wa skauti kuhusu kuzuia na kupambana na rushwa ili wawe washiriki wa kuzuia na kupambana na rushwa kuanzia kwao binafsia, ngazi ya shule, familia, jamii na Taifa kwa ujumla.
“Katika malalamiko yanayohusu rushwa yapo kwenye hatua mbalimbali za uchunguzi,” amesema Makungu.
Amesema kesi tano zimefunguliwa mahakamani zenye washtakiwa 10 na kuongeza idadi ya kesi zilizopo mahakamani kuwa 44.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment