Ajinyonga Kisa Msongo Wa Mawazo


Na Lucas Raphael,Tabora
Kijana wa Miaka 18, Michael  Paulo mkazi wa Mtaa wa Luanzari Kata ya Ngambo Manispaa ya Tabora amekutwa amejiua kwa kujinyonga kwa kutumia shuka kutoka na msongo wa mawazo.

 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora ACP Richard Abwao inasema kuwa Kijana Paulo aligundulika akiwa amefaiki kwa kujinyonga kwa kutumia shuka kwa kujitundika kwenye Kenchi ndani ya chumba chake Oktoba 24/2021 saa saba mchana.

Kamanda Abwao aliongeza kuwa taarifa ya kifo hichp ilitolewa kituo cha polisi na Dada wa Marehemu aliyejitambulisha kwa jina laJane Paulo.

Dada huyo wa Marehemu aliwambia polisi kuwa kabla ya tukio hilo aliacha ujumbe wa maandishi uliosomeka kwamba “  Mama Naomba Unisamehe ni Maisha tu Yamenifanya Nijiue Mnizike “.

Kamanda Abwao alisema kuwa uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha kifo hicho ni Msongo wa Mawazo na mbinu aliyotumia ni kujifungia chumbani na kisha kujitundika kwa kutumia shuka.

Alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora Kitete kwa ajili ya kufanyiwa uchungzi wa Kitabibu.

Kufuatia tukio hilo Kamanda Abwao anatoa Rai kwa wananchi kutojichukulia maamuzi Magumu yaliyo kinyume na Sheria na kwamba wanapokutana na Changamoto ni vizuri kushirika Jamii na Viongozi wa dini.

MWISHO.



from MPEKUZI

Comments