RC Makalla Aagiza Polisi Kuanza Operesheni Ya Kukamata Wezi Wa Vifaa Vya Magari Na Vibaka Dar es Salaam


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amelielekeza Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam kuanza msako wa kuwabaini na kuwakamata Wezi wa Vifaa vya Magari Na vibaka na kuwachukulia hatua Kali za kisheria.

RC Makalla ametoa maelekezo hayo wakati wa Kikao Cha tathimini ya ziara yake ya kusikiliza Migogoro Jimbo kwa Jimbo ambapo amesema kumeanza kuibuka vitendo vya Wizi na kuleta taharuki kwa Wananchi jambo ambalo hawezi kulifumbia macho.

Aidha RC Makalla ametoa wito kwa wazazi kuchunguza mienendo ya watoto wao na kuwakanya ili wasijekuingia kwenye mikono ya Vyombo vya dola.

Agizo hilo limetolewa kwa mikono miwili na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es salaam Muliro Jumanne ambae amewaelekeza makamanda wote wa Mikoa ya kipolisi kuanza kazi ya kuwasaka wahalifu Mara moja.



from MPEKUZI

Comments