Sababu ya Mwili wa Hamza Mohammed kuzikwa usiku yatajwa

Mwili wa Hamza Mohammed aliyefariki katika majibizano ya risasi kati yake na Polisi umezikwa jana  Jumapili August 29, 2021 usiku  katika makaburi ya Kisutu.

Mwili huo ulizikwa baada ya kuswaliwa katika Msikiti wa Mamuur uliopo Upanga jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Msemaji wa familia ya , Abdulrahm Hassan, amesema kuwa awali mwili huo ulitarajiwa kuzikwa saa 7:00 mchana katika makaburi hayo, lakini  ulichelewa kwa sababu ya kazi ya kutoa risasi zilizokwama kwenye mwili wake.

Hamza alizua taharuki siku ya Agosti 25, 2021, baada ya kuwauwa kwa risasi Askari wanne akiwemo mmoja wa Kampuni ya Ulinzi binafsi ya SGA maeneo ya daraja la Selander karibu na zilipo ofisi za Ubalozi wa Ufaransa wilayani Kinondoni.



from MPEKUZI

Comments