Ajali Ya Gari La JWTZ, Lori La Mizigo Yaua Watu 10 Geita


Watu 10 wamefariki dunia na wengine 4 kujeruhiwa kwenye ajali iliyotokea  jana Kijiji cha Ilalwe kata ya Bukombe mkoani Geita iliyohusisha  Gari la jeshi la wananchi na gari aina ya Scania T130 DRZ lililokuwa limebeba mzigo likitokea Dar es Salaam kuelekea nchini Rwanda.

Akizungumzia tukio hilo, Mkuu wa wilaya ya Bukombe, Said Nkumba amesema majeruhi 6 wamepelekwa katika Hospitali ya Ushirombo na wawili wapo kituo cha afya Masumbwe wakiendelea kupatiwa matibabu huku chanzo cha ajali hiyo kikiwa hakijafahamika.



from MPEKUZI

Comments