TECNO Yatoa Shukrani Kwa Wateja Wake.


Kampuni ya simu za mkononi TECNO wakishirikiana na Tigo Tanzania wamekamilisha kampeni yao ya kusherehekea awamu ya kwanza ya Camision Camping Kistaa na TECNO Camon 17 2021 kwa hafla kubwa iliyofanyika mwisho mwa wiki iliyopita.


Shamrashamra za maadhimisho hayo zilisindikizwa na pongezi kwa washindi zaidi ya 30 wa promosheni ya Camision Camping Kistaa na TECNO Camon 17 na miongoni mwao ni Patrick Alsina kijana mwenye kipaji cha kuimba ambacho bado hakijapata nafasi ya kusikiwa na wengi, Razack Mbaga kijana anayejishughulisha na upigaji picha walijishindia nafasi ya kwenda kutembelea Mbuga za Wanyama Mikumi wakiongozana na jopo la washindi wengine bila ya kusahau Yusuph Yusuph Mjasiriamali anayejishughulisha na biashara ya utembezaji magazeti barabarani alijishindia Jokofu huku washindi wengine wakijishindia ving’amuzi vya DSTV na Drones.

Washindi wote waliopatikana kwenye promosheni hii walianza kwanza kwa kununua TECNO Camon 17 kabla ya kuingia kwenye droo kuu lililochezeshwa na msanii Elizabeth Michael siku mbili kabla ya hafla kubwa ya iliyofanyika Mbuga ya Wanyama Mikumi. 


Wakati wa makabidhiano wa zawadi hizo yaliyofanyika katika duka la TECNO Smart Hub Kariakoo, Elizabeth Michael alisema, “TECNO Camon 17 ni simu yenye kusifika kutokana ubora wa Kamera zake mbele ikiwa na MP48 na nyuma ikiwa MP64 ambazo ni hodari kwa upigaji picha ang’avu na zenye rangi halisi kulingana eneo na muda wa uchukuaji picha”.


Kampeni hii iliendeshwa na TECNO wakiwa kama wahusika wakubwa kwa kushirikiana na DSTV, Tigo kwa dhumuni la kuboresha na kupunguza gharama zinazotokana na upatikanaji wa habari kupitia mifumo ya kidigital Tigo imelisimamia hili kupitia ofa ya GB78 za internet zinazopatikana kwenye simu za TECNO Camon 17.


Sherehe hizo za maadhimisho zilipambwa pia na matukio mengine ikiwemo mashindano ya kuimba, kucheza, kuchekesha n.k vile vile wageni waalikwa ambao ni wasanii maarufu Jihan Mark na Idrissa Sultan walipata wasaa wa kupiga picha, kula pamoja na kujuana na mashabiki wa kazi zao za sanaa.


TECNO inawashukuru watanzania wote kwa mapokezi mazuri ya TECNO Camon 17.





from MPEKUZI

Comments