Waziri Lukuvi Azitaka Taasisi za Serikali Kutenga bajeti ya fidia kabla ya kutwaa maeneo


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amezitaka wizara, taasisi na mamlaka mbalimbali kuhakikisha zinatenga bajeti kwa ajili ya kulipa fidia kabla ya kutwaa ardhi kutoka kwa wananchi.

Lukuvi ameyasema hayo leo Jumatano Mei 26,2021 wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka 2021/22.

Amesema jumla ya migogoro ya ardhi 3,171 ilipokelewa kupitia programu ya Funguka kwa Waziri ambapo hadi kufikia  Mei 15,  2021 migogoro 1,144 ilishughulikiwa.

Amebainisha kuwa kati ya migogoro hiyo asilimia 39 inahusu masuala ya fidia.


from MPEKUZI

Comments