Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shaka amekabidhiwa ofisi na aliyekuwa Mkuu wa Idara hiyo, Humphrey Polepole, huku akisisitiza kuwa chama kipo imara.
Makabidhiano ya ofisi hiyo yamefanyika jana katika ofisi za CCM ofisi Ndogo Lumumba jijini dar es salaam na kuhudhuriwa na baadhi ya viongozi .
Katika makabidhiano hayo shaka amesema chama Cha mapinduzi bado kipo imara na kitaendelea kuwa imara kutokana na uongozi madhubuti wa mwenyekiti wa CCM Rais Samia Suluhu Hassan.
Kupitia Idara hiyo shaka amesema atatumia weledi wake na uzoefu ndani ya chama katika kuenezi Itikadi ya chama nchi nzima ikiwemo kupata wanachama wapya na kueneza siasa Safi.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment