Kampuni ya simu TECNO imezindua rasmi promosheni ya SUPA FRIDAY jana katika duka la TECNO Smart Hub lililopo Kariakoo. Uzinduzi huo uliudhuriwa na wageni waalikwa mbalimbali kutoka kwenye kiwanda cha Sanaa kama vile Elizabeth Michael, Idrisa Sultan, Angel Nyigu na Jihan Mark.
Promosheni ya SUPA FRIDAY itakuwa ikifanyika kila ijumaa na ambapo simu za TECNO Camon zitakuwa zikiuzwa kwa bei pungufu lakini pia zawadi mbalimbali kutolewa kama vile Fridge, Drones, DSTV Decoder na zawadi nyenginezo kama ticket yakwenda kutembelea Mbugani.
Wakati wa uzinduzi huo Msanii maarufu kutoka kwenye kiwanda cha filamu alisema, “simu ni kamera na TECNO wamelizingatia hilo kwenye simu hii ya TECNO Camon 17, naipenda sana simu yangu MP48 za selfie na MP 64 za kamera ya nyumba zinanifanya nionekane mrembo wakati wote ningependa nikushauri wewe mfanyabiashara kupitia mitandao ya kijamii nunua TECNO Camon 17pro kwani picha zake zinaendana na uhalisia wa bidhaa yako inavyoonekana”.
Lakini pia wateja walioenda kununua simu siku ya jana walikuwa na haya yakusema kuhusiana na bidhaa na promosheni ya SUPA FRIDAY, “Tunaishukuru sana kampuni ya simu TECNO imekuwa ikizingatia wateja wake wote hadi sisi wenye uchumi mdogo lakini tungetamani kumiliki simu ya TECNO Camon 17, SUPA FRIDAY imetimiza ndoto zangu kupitia ofa ya punguzo la bei na mimi sasa namiliki TECNO Camon 17 sasa nina uwezo wakuhifadhi picha, video na files nyengine kibao GB128 kwa 8ram zinanitosha kabisa sihitaji memory ya ziada alisikika akisema moja wa wateja wa TECNO Camon 17”.
TECNO Camon 17 inapatikana katika maduka yote ya simu ikiambatana na ofa ya GB78 za bundle la internet kutoka Tigo.
Tembelea www.tecno-mobile.com
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment