Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, anayeshughulikia Maendeleo ya Jamii Mwanaidi Ali Khamis amesema Serikali itaendelea kutenga Bajeti kwa ajili ya kutoa huduma zote za msingi kwa wazee wasiojiweza ikiwa ni pamoja na matibabu, chakula, mavazi na huduma nyingine za msingi.
Naibu awaziri Mwanaidi ameyasema hayo leo alipotembelea Makazi ya Wazee wasiojiweza Nunge yaliyopo Wilaya ya Kigamboni Mkoa wa Dar es Salaam ambapo amesisitiza kuwa Serilikali itahakikisha Wazee katika makazi wamepata huduma muhimu.
Amesema kuwa Serikali inatambua kuwa, wazee ni tunu na hazina kubwa kwa ustawi na maendeleo Tanazania na hivyo, mchango wao lazima uenziwe law kila namna.
“Nipende kuwahakikishia kuwa huduma hizi zitaendelea kuboreshwa na kutolewa kwa utoshelevu ili kuwafanya wazee wetu mnafurahie matunda ya jitihada kubwa mlizozifanya kwa nchi yetu” alisema Naibu Waziri.
Aidha, amefafanua kuwa Serikali imeshaanza kushughulikia baadhi ya changamoto zinazowakabili wazee wanaoishi kwenye makazi hayo ikiwemo ukarabati miundombinu na nyumba 10 za makazi 10 ya Wazee.
Amesema Serikali itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya Ujenzi wa Uzio kuzunguka makazi hiyo ili kuimarisha usalama wa Wazee na mali zao.
Kwa upande Mkuu wake Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sara Msafiri akimkaribisha Naibu Waziri kuzungumza na Wazee hao, alieleza kuwa changamoto kubwa imekuwa ni kukosa uzio ili kuwaepusha na uvamizi wa makazi ya watu na vifaa vyao.
Kwa upande wao, baadhi ya Wazee wanaoishi hapo, Magreth Abdalla, Mzee Ubwabwa na Mzee Ali wamemshukuru Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na Serikali yake kwa kuendelea kuwakumbuka na kuwahudumia.
” Tunashukuru sana kwa kutusalimia na kutuletea zawadi, tunamshukuru Mama Samia kwa kuendelea kutukumbuka na alishatutembelea, tunaamini changamoto zilizopo zitafanyiwa kazi” alisema Mzee Ubwabwa.
Akihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jijjni Dodoma Aprili 22, mwaka huu, Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan alitaja huduma kwa Wazee kuwa ni miongoni mwa Vipaumbele vya Serikali anayoiongoza.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment