Rais mstaafu Jakaya Kikwete: Sitarajii Uenyekiti,Urais CCM utenganishwe


Rais  mstaafu Jakaya Kikwete amesema hatarajii utamaduni tofauti kutumika na Chama cha Mapinduzi kuitenganisha kofia ya uenyekiti wa chama na urais kwa kuwa suala hilo halina afya kwa chama hicho na nchi kwa ujumla.

Kikwete aliyasema hayo alipozungumza na chombo kimojawapo cha habari nchini ikiwa imesalia siku nne tu kabla ya kufanyika Mkutano Mkuu Maalum wa Chama cha Mapinduzi.

“Mimi sifikirii kwamba kutakuwa na utaratibu tofauti na tukitengeneza utaratibu huo tofauti utakuwa hauna maslahi kwa chama na taifa…busara iliyotumika kutotenganisha kofia mbili (urais na uenyekiti wa chama) iendelee kutumika”-alisema Kikwete .

Kikwete amesema busara hiyo inayotumika toka zamani kutotenganisha kofia mbili ni vyema ikaendelea kutumika ili kuepusha chama na  nchi kuyumba pale Mwenyekiti wa chama anapotofautiana na Rais.

“Wakitofautiana hawa Chama kinayumba, nchi inayumba .Mimi nadhani busara ile iendelee kutumika…hatukukubaliana kutenganisha huku juu, tulikubaliana huku juu kutabaki hivyo hivyo.Na huku chini tulikotenganisha unaona ,wakati mwingine mkuu wa mkoa na katibu wa mkoa hawaelewani , katibu wa wilaya na mkuu wa wilaya hawaelewani” alisema Kikwete




from MPEKUZI

Comments