Daniel Chongolo ateuliwa Katibu Mkuu CCM


Chama cha Mapinduzi  CCM kimemteua mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo kuwa katibu mkuu wa chama hicho tawala kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Dk Bashiru Ally.

Chama hicho pia kimemteua Christina Mndeme kuwa naibu katibu mkuu Bara huku  Abdallah Juma Sadala akiendelea kuhudumu nafasi hiyo upande wa Zanzibar

Katibu wa itikadi na uenezi iliyokuwa ikishikiwa na Humprey Polepole, sasa itashikiliwa Shaka Hamidu Shaka na katibu wa uchumi na fedha ni Frank Hawasi.



from MPEKUZI

Comments