Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu Serikali, Charles Kichere amesema Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) limetengeneza hasara ya Shilingi bilioni 60 kwa mwaka na kwa kipindi chote cha miaka ya nyuma shirika hilo limekuwa likijiendesha kwa hasara.
CAG, Kichere amebainisha hayo wakati wa uwasilishaji wa ripoti yake kwa mwaka wa fedha 2019/2020 kwa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, hafla iliyofanyika Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma hii leo.
“Katika ukaguzi wetu wa mwaka 2019/2020 tumegundua Shirika letu la Ndege limetengeneza hasara mwaka huu ya Tsh bilioni 60 ila kwa miaka mitano pia limekuwa likitengeneza hasara, kuna changamoto ambazo Serikali inabidi iziangalie ili Shirika letu litekeleze majukumu yake vizur,”alisema Kichere.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment