NMB Bonge la Mpango; Jishindie hadi Sh. Milioni 500/-

Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara wa Benki ya NMB, Filbert Mponzi akizindua rasmi kampeni ya Bonge la Mpango inayowazawadia  wateja pesa taslimu, pikipiki za miguu mitatu , gari ya mizigo alimarufu Kilikuu na Toyota Fortune mpya. Wakishangilia ni baadhi ya  viongozi wa Benki ya NMB.
Aina tatu ya Zawadi zinazoshindaniwa ndani ya bonge la Mpango; Pikipiki za miguu mitatu , gari ya mizigo alimarufu Kirikuu na Toyota Fortune mpya.








Benki ya NMB imeizindua kampeni inayojulikana kama ‘Bonge la Mpango’ ambayo itawawezesha wateja kushinda fedha taslimu, Pikipiki ya Miguu mitatu, gari aina ya Tata - Kirikuu na gari ya kifahari aina ya Toyota Fortuner.

Katika kampeni hiyo, zaidi ya TZS 550 milioni zitatumika kutoa zawadi kwa washindi, huu ukiwa ni mkakati wa Benki ya NMB kwa mwaka 2021 unaokusudia kuendelea kuifanya NMB kuwa chaguo la kwanza kwa wateja kwa usalama wa fedha zao pamoja na uhakika wa huduma nyingine za kibenki.

Wateja wote wa NMB wanaofika zaidi ya Milioni Tatu nchini wana nafasi ya kushinda zawadi wakati mshindi wa mwisho atajinyakulia Toyota Fortuner mpya kabisa (kilomita sifuri) yenye thamani ya shilingi milioni 169.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo, Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara, Filbert Mponzi alisema ni hii ni moja ya njia za kurudisha faida kwa wateja wao waaminifu wanaotunza fedha ndani ya benki hiyo huku ikikusudia kuhamasisha utamaduni wa kutunza akiba kwa ajili ya matumizi ya baadaye. 

Katika kipindi chote cha kampeni hii, alisema wateja wao wanaoweka akiba ya walau TZS 100,000 wataingia kwenye orodha ya wanaostahili zawadi zilizopo ambazo ni fedha taslimu shilingi 500,000 kwa washindi 10 kila wiki, Pikipiki ya kubebea mizigo aina ya LIFAN, Gari ya kubebea mizigo maarufu kama Kirikuu au Toyota Fortuner. Kampeni hiyo itaendelea mpaka Mwezi Mei mwaka huu.

“Tunatoa fursa kwa wateja wetu sambamba na kuwahamasisha kujenga utamaduni wa kujiwekea akiba hasa kipindi hiki ambacho kila mmoja anaugulia maumivu ya msimu wa sikukuu za mwisho wa mwaka uliomaliza fedha,” alisema Bwana Mponzi.

Kampeni hii pia inalenga kuwahamasisha wasio na akaunti ya benki nchini kuja kufungua na kutunza akiba zao kwa njia salama zaidi na benki ya NMB.Ikiwa benki inayoongoza nchini, NMB Inakusudia kuhamasisha utamaduni wa kujiwekea akiba. Umuhimu na thamani ya kampeni hii utathibitisha jinsi benki hiyo inavyowajali wateja wake bila kuwasahau wananchi wasiotumia huduma za benki.

Ili kukidhi vigezo na sifa za kujishindia zawadi zitakazotolewa, mteja anatakiwa kuweka akiba kwenye akaunti yake. Mteja atakayefungua akaunti na kuweka akiba ya TZS 100,000 au zaidi iwe kwa fedha taslimu au kuhamishia kwenda akaunti yake ya Benki ya NMB anajiweka kwenye nafasi ya kushinda zawadi zitakazotolewa kila wiki na atakuwa sehemu ya watakaoshindania zawadi ya mwezi itakayotoa washindi watatu wa Gari ya Mizigo - Kilikuu au Pikipiki ya Mizigo aina ya LIFAN.

Droo ya mwisho itawahusisha wateja ambao wana akiba ya zaidi ya TZS 10 milioni kwenye akaunti zao iliyodumu kwa zaidi ya siku 30. Wateja hawa wanaweza kujishindia gari aina ya Toyota Fortuner yenye thamani ya TZS 169 milioni.




from MPEKUZI

Comments