Dk. Ndugulile alisema lengo la Rais John Magufuli kuunda wizara maalum ya TEHAMA ni kuifikisha Tanzania kwenye ulimwengu wa teknolojia hivyo ipo kazi kubwa ya taasisi kuondokana na mazoea ya utoaji huduma kwa wananchi.
“Nitoe rai kwa benki nyingine, kuiga sio dhambi... nao waige kwa Benki ya CRDB yaani mteja anauwezo wa kufanya kila kitu kinachohusu akaunti yake na zaidi akiwa na simu yake ya mkononi.
“Benki ya CRDB wamenifariji zaidi baada ya kujua kwamba ubunifu wa huduma hii umefanywa na vijana wa kitanzania yaani ‘local services’ hili nalo ni jambo la kupongeza sana.
“...Hata serikali hivi sasa inawafuata wananchi kwa kuhakikisha masuala yote ya malipo ya serikali yanafanyika kwa simu za mkononi,” alisema Dk. Ndugulile ambaye pia ni Mbunge wa Kigamboni.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema lengo la taasisi hiyo kubwa ya fedha hapa Tanzania ni kumfikia mwananchi popote alipo kwa kutumia mifumo ya kidijitali.
Nsekela alisema kupitia SimBanking mpya wateja sasa hivi wanafanya kila kitu kidijitali, kuanzia kufungua akaunti wenyewe kidijitali, kuomba mkopo kidijitali, kulipia bima kidijitali, kulipia ankara kidijitali na huduma nyengine lukuki. “… tumefanya maboresho makubwa sana ambayo yanampa uhuru mkubwa mteja wa kufanya miamala yote kupitia SimBanking na ndiomana sasa hivi tunasema Benki ni SimBanking,” aliongezea Nsekela.
Naye Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA), Khadija Said aliipongeza Benki ya CRDB kwa ubunifu bora wa huduma za kiteknolojia na kuwawezesha wateja wa benki hiyo kukata bima mbalimbali kwa kutumia simu ya mkononi. Naibu Kamishna aligusia pia kuhusu upatikanaji wa huduma ya stika za bima za magari kidijitali kupitia SimBanking pindi stika hizo zitakapozinduliwa rasmi mwezi Aprili.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment