Tangazo la Nafasi za Masomo Chuo Kikuu Kishiriki Cha Kumbukumbu ya Stefano Moshi (SMMUCo)


Chuo Kikuu Kishiriki Cha Kumbukumbu ya Stefano Moshi (SMMUCo) kinatangaza nafasi za masomo kwa mwaka 2021/2022 katika ngazi ya Cheti na Diploma zinazotolewa na Taasisi Tanzu ya Masoka Professionals Training Institute iliyopo Moshi Mjini, Kozi hizi zitaanza mwezi Machi, 2021.

Nafasi ni kwa kozi zifuatazo:

1. Business Administration

2. Records and Archives Management

3. Accountancy

4. Community Development

5. Journalism

6. Procurement and Supply

  

SIFA ZA MWOMBAJI

Kozi za Cheti: Mwombaji awe amehitimu kidato cha nne awe na ufaulu wa alama D nne na kuendelea isipokuwa somo la Dini.

Diploma: Mwombaji awe amemaliza kidato cha sita na awe na Principal Pass moja na subsidiary moja isipokuwa somo la Dini AU awe amehitimu cheti (astashahada) kutoka Chuo kinachotambulika na Serikali.

Chuo pia kinatangaza nafasi za ufadhili wa nusu ada kwa waombaji wanaotoka katika sharika zote za KKKT Dayosisi ya kaskazini. Hivyo wote wenye sifa wanahimizwa kufika kwa wachungaji wao ili kusajiliwa katika mpango huu maalumu.

Pia Chuo kinatoa Mikopo ya Elimu isiyokuwa na Riba kwa watu wote kupitia SACCOS ya KKKT Dayosisi ya Kaskazini kwa yeyote atakayesoma au kumsomesha mwanae/ndugu katika chuo cha SMMUCo.

Maombi yanaweza kufanyika kwa njia ya mtandao kupitia tovuti ya chuo: www.smmuco.ac.tz

 

FOMU ZINAPATIKANA SEHEMU ZIFUATAZO

1. Tovuti ya Chuo: www.smmuco.ac.tz

2. Chuoni - Moshi Mjini

4. KKKT Christian Bookshop Moshi Mjini – mkabala na stendi kuu ya mabasi

5. Ofisi za Sharika zote.

Kwa maelezo zaidi: Piga simu namba: 0653422928, 0756512757, 0786862089, 0756029652

 

NYOTE MNAKARIBISHWA



from MPEKUZI

Comments