Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amewataka Polisi Wasaidizi waliopo kwenye taasisi mbalimbali nchini kuhakikisha wanaheshimu na kuzingatia sheria sambamba na nidhamu wakati wanapotekeleza majukumu yao ya kazi za kila siku katika kubaini, kuzuia na kupambana na uhalifu.
IGP Sirro amesema hayo jana jijini Dar es salaam, wakati alipofanya kikao kazi na Polisi Wasaidizi waliopo Kanda Maalum ya Dar es salaam ambapo amesema kuwa, weledi, ufanisi na kujituma kutasaidia kupunguza malalamiko miongoni mwa jamii wanayoihudumia.
Naye Kamishna wa Kamisheni ya Ushirikishwaji wa Jamii Dkt. Mussa Ali Mussa amesema kuwa, uwepo wa Polisi Wasaidizi umesaidia kuwezesha mamlaka na Halmashauri mbalimbali zilizopo nchini kuendelea kuimarika.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment