Dereva wa basi akatisha uhai wa mwalimu.


Samirah Yusuph
Maswa.
Gari la abiria lenye namba za usajili T 423 DKN  mali ya kampuni ya Ally's star limemgonga na kumsababishia kifo Muhoni Zakayo Daffi(52), ambaye ni mwalimu wa shule ya sekondari Salange iliyopo Malampaka wilaya ya Maswa.

Ajali hiyo imetokea katika kijiji cha Isulilo barabara ya Maswa,Shinyanga majira ya  saa nne usiku wa Januari, 27 wakati Mwalimu huyo akielekea katika kituo chake cha kazi katika kijiji cha Salange Malampaka.

Akithibitisha taarifa hizo kamanda wa jeshi la polisi Mkoa wa Simiyu Richard Abwao amesema kuwa gari hilo lilokuwa likitokea Shinyanga kwenda Bariadi likiendeshwa na Erasto Onesphory Chami(37) lilimgonga na kumsababishia kifo mwalimu huyo alipokuwa akiendesha pikipiki.

"Chanzo cha ajali ni matumizi mabaya ya barabara yaliyofanywa na dereva wa basi ambaye alihama upande wa kushoto kwenda wa kulia kwa ajili ya kulipita gari lingine lililokikuwa mbele yake bila kujali kuwa kuna mtumiaji mwingine wa barabara mbele," Alisema Abwao.

Aidha ameongeza kuwa Mwili wa marehem umehifadhiwa katika hosipitali ya wilaya ya Maswa na jeshi la polisi linamshikilia dereva wa basi pamoja na basi lililofanya ajali hiyo katika kituo cha polisi Maswa.

Mwisho.


from MPEKUZI

Comments