Na Amiri Kilagalila, Njombe
RAINARY Lugome mkazi wa wilaya ya Ludewa mkoani Njombe ameuawa na ndugu yake aliyefahamika kwa jina la Claus Samweli Lugome (46) kwa tuhuma za kuku wake kuingia katika shamba la kaka yake.
Akizungumza na vyombo vya habari kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa amesema wanawashikilia wanafamilia wawili akiwemo baba wa watoto hao, Ado Samweli Lugome pamoja na kijana aliyehusika na mauaji kwa ajili ya upelelezi.
“Haya mauaji ni ya hovyo,yaani kaka kamuua mdogo wake kisa na mkasa kuku wa mdogo mtu wameenda kwenye shamba la kaka mtu.”Alisema Kamanda Issa
Hata hivyo ameongeza kuwa katika upelelezi uliokuwa unaendelea wamebaini familia hizo zimekuwa zikituhumiana na maswala ya ushirikina.
“Katika ufuatiliaji wa swala hili tumeona wanatuhumiana kuwa mmoja anatembea na mke wake na mwingine anamtuhumu mwenzie kuwa alikuwa anamloga.”Alisema kamanda Issa
Ametoa rai kwa jamii kuacha kuamini ushirikina badala yake kutoa taarifa sehemu husika ili kusaidiwa kuliko kuchukua hatua mkononi.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment