TECNO Na Manchester City Kuwazawadia Mashabiki Zawadi Mbalimbali.

 Mwaka 2020 umekuwa mwaka wa changamoto karibu kwa kila mtu. Kwa kuwa sote tutasherehekea moja ya vipindi bora vya mwaka, TECNO itakuwa ikifanya kitu tofauti mwaka huu kwa kuwapa kitu bora mashabiki wao kwa kuongeza shauku na ujasiri katika mwaka mpya. Kwa kutumia hashtag za “#HeadIntoTheNewYear” na “#CelebrateDifferent” pamoja na kushiriki kwenye kurasa rasmi za mitandao ya kijamii za TECNO unapata nafasi ya kushinda zawadi kibao!


Ili kusherehekea kuelekea Mwaka Mpya, wafuasi wa Simu za Mkononi za TECNO watapata nafasi ya kushinda zawadi nzuri wakati wowote ambapo Manchester City itacheza kwenye msimu huu wa sikukuu.

 
Kwa kushirikiana na washirika wake Manchester City, TECNO inawataka mashabiki wanaoshiriki kote Afrika Mashariki, Afrika Magharibi na Kusini Mashariki mwa Asia kuonyesha jinsi watakavyosherehekea kitofauti msimu huu wa sikukuu na kuelekea Mwaka Mpya, hivyo kila wakati Manchester City inapofunga bao au inaposhinda mchezo, wafuasi wa TECNO wanaweza kuonyesha furaha yako kwa kutumia hashtag hizo na huwenda na wewe ukushinda pia!

 
Basi hebu tuonyeshe jinsi utakavyosherehekea magoli na ushindi wa Manchester City msimu huu wa Sikukuu kwa njia yoyote unayotaka kuelezea. Inaweza kuwa video ya wewe na familia yako mkishangilia nyumbani, picha ya wapi unatazama, au hata hadithi ya kwanini mchezo fulani una maana kubwa kwako. Chaguo ni lako!

 
Mbali na zawadi zitakazo tolewa, video bora, hadithi, au picha zitaonyeshwa kwa baadhi ya wachezaji wa Manchester City hapo Januari mwaka 2021, ambao ndio wataamua video, hadithi au picha bora - kwa hivyo uwe mbunifu iwezekanavyo na maingizo yako ikiwa unataka kutambuliwa! Huwezi kujua, unaweza kuwavutia tu na lolote linaweza kutokea!


Eric Mkomoye, Afisa Mahusiano TECNO alitoa maoni yake juu ya uzinduzi wa shindano hilo, "Ulimwengu utakuwa ukisherehekea “kitofauti” katika kipindi hiki cha sikukuu, katika kila mwendo wa maisha na haswa ndani ya mpira wa miguu. 

Kampeni yetu inamtaka kila mtu aingie mwaka mpya "kitofauti" kwa kuchochea ubunifu na kuleta mshangao zaidi kwenye maisha. Tunataka mashabiki wetu kuchukua hatua ya kuwa katikati kwa njia halisi inayohusiana moja kwa moja na ushirikiano wetu na Manchester City, na kuonyesha msingi halisi wa kampuni ya TECNO na bidhaa zake. Kwa ufupi unaweza kusema, tunataka kuhamasisha zaidi wateja wetu na kuwazawadia kwa kushiriki.”

 
Sio tu unaweza kushiriki mtandaoni, unaweza pia kushiriki katika maduka ya TECNO yaliyo chaguliwa  na yenye shughuli za mpira wa miguu ndani ya duka katika mikoa yote. Uliza tu rafiki au mfanyikazi wa TECNO ukiwa ndani ya duka kukuchukulia filamu au picha ikionyesha unavyoshiriki kwenye moja ya michezo yetu ya ' Head into the New Year’. 

 
Tag TECNO Mobile ukitumia hashtag za #HeadIntoTheNewYear #CelebrateDifferent kwenye mitandao ya kijamii ili kushinda. Zawadi za papo hapo zitapatikana dukani, na pia utaingizwa kwenye shindano kuu ukituma picha yako kwenye mitandao ya kijamii.

 
Kwa hivyo, toa simu yako na utuonyeshe jinsi utakavyokuwa ukielekea mwaka mpya kwa kusherehekea msimu huu wa sherehe!

 
Kwa maelezo zaidi tembelea ukurasa huu - https://bit.ly/39XeDjb



from MPEKUZI

Comments