NA DENIS MLOWE, IRINGA
MKURUGENZI Mkuu wa TAKUKURU nchini, Brigedia Jenerali John Mbungo ametoa siku 14 kwa wakandarasi wa makampuni 16 waliokuwa wanaotekeleza miradi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) nchini kuhakikisha wanakabidhi vifaa ghafi kwa tanesco kutokana na mikataba waliyofikiana.
Akizungumza wakati wa kuwakabidhi shirika la umeme nchini (TANESCO) vifaa ghafi vyenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 1. 2 vilivyookolewa kutoka kwa mmoja ya wakandarasi ,Brigedia Jenerali Mbungo alisema kuwa makampuni 16 yanatakiwa kukabidhi vifaa ghafi hivyo kuanzia Leo kwa mujibu wa mikataba yao.
Alisema kuwa licha ya kukumbushwa mara kwa mara kufanya urejeshaji huo na kupewa NOTISI ya kufanya hivyo mwaka 2017 wameshindwa kukabidhi vifaa ghafi hivyo kwa tanesco hivyo siku 14 kuanzia Leo wahakikishe wanakabidhi.
Alisema kuwa Vifaa ghafl vilivyokabidhiwa kwa shirika hilo mkoa wa Iringa vimetokana na Operesheni ya uchunguzi wa Miradi ya REA II iliyofanyika katika mkoa wa Iringa.
Alivitaja Vifaa ghafl hivyo ni pamoja na Transfoma 34 zenye ukubwa tofauti, Mita za LUKU 1,458 na vifaa vyake, Nyaya zenye urefu wa km 70.8 pamoja na Vifaa 3O vya umeme (Ready boards) vya aina tofauti tofauti vyote vikiwa na thamani ya shilingi Bilioni Moja, Milioni Mia Mbili Kumi na Sita, Laki Nane na Arobaini, Mia Tatu na Sitini(1,216,840,360.)
Brigedia Jenerali Mbungo aliyataja makapuni hayo yanayotakiwa kurejesha vifaa ghafi na kupelekewa notisi na REA tangu mwaka 2017 lakini bado hawajawasilisha vifaa ghafi hivyo katika ofisi za TANESCO
Wakandarasi hao ni Shandong Taikai Power, EngineerinCo. Ltd, Angelique International Limited ,Dermgggtrics T Ltd, Lucky Exports (Energy Division) na Spencon Services Limited.
Wakandarasi wengine ni LTL Pro’ects PVT Limited , Namis Cor-orate Ltd , O K Electrical & Electronics Services Ltd, China Henan International Co corporation Group Co. LTD , China National Electrical Wire & Cable States Grid Electrical & na kuongeza Technical Works Ltd; M.F Electrical Engineering Ltd, Vayer General &TD L’Imlted, DIEYNEM Co Limited na GESAP Electrical Sunlies Co. Ltd CC; International EpuneerinNiceria Smotec Co. Ltd 7 STEG Internati m Services onal
Alisema kuwa baaada ya kuwapa siku hizo kumi na nne wakashindwa kurejesha vifaa ghafi hivyo watahakikisha wanawakamata na kuwashughulikia kwa mujibu wa Sheria.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tanesco nchi, Dk. Tito Mwinuka licha ya kuishukuru taasisi ya Takukuru aliipongeza kwa kuwa mstari wa mbele katika kutimiza majukumu yake.
Aliwataka wakandarasi wanaotekeleza miradi ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kutimiza wajibu wao kwa wakati muafaka.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment