Moto umeunguza maduka zaidi ya 10 na kuteketeza baadhi ya vitu ni katika majengo yanayomilikiwa na familia ya Nekemia Kazimoto (Kazikomu) yaliyopo Mji wa kayanga mjini, Karagwe, Kagera mkabara na majengo ya city center na Magereza ya kayanga.
Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Godfrey Mheluka aliongoza wananchi kuzima moto huo ambao uliibuka saa 5 na dakika 20 usiku katika moja ya duka la nguo na kusambaa katika maduka mengine ya bidhaa za vyakula, hoteli, stoo za vifaa vya ujenzi, salooni na maduka ya bidhaa mchanganyiko.
Mheluka amesema kuwa chanzo cha moto huo hakijafahamika mpaka sasa.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment