Serikali yatoa ufafanuzi wa hoja, ajira mpya za waalimu


 Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandisi Joseph Nyamhanga, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimeti ya utumishi wa umma na utawala bora Dkt. Laurean Ndumbaro na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo wametoa ufafanuzi juu ya hoja mbalimbali zilizojitokeza kwenye ajira mpya za waalimu.

Ufafanuzi huo umetolewa leo katika Ofisi ya Rais – TAMISEMI Jijini Dodoma  mara baada  kutokea hoja mbalimbali katika mitandao ya kijamii na vyombo vya habari  kuhusu ajira  mpya za walimu zilizotangazwa hivi karibuni.

Amesema ajira  hizo zilitangazwa  baada ya kukamilika kwa mchakato  wa uchambuzi  wa maombi  ya ajira  uliofanywa  na Ofisi ya Rais  TAMISEMI  kwa kushirikiana  na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi  wa umma  na utawala bora na  tume  ya utumishi wa walimu.

Mhandisi Nyamhanga  amesema hoja kubwa ilyojitokeza ni kwa jina la  Mwalimu mmoja kujitokeza katika kila ukurasa na kuonekana mara 196, badala ya mstari wa  maelezo ya Jedwali (Sub- titles) lakini shule aliyopangiwa ni moja, pamoja na jina hilo kujirudia  halikuchukua nafasi   ya mwombaji  yoyote  ya walimu waliotakiwa kuajiriwa au kuathiri  idadi ya waalimu  waliotakiwa kuajiriwa na  tayari marekebisho yamefanyika.

Mhandisi Nyamhanga amefafanua kuwa Shule binafsi kupangiwa mwalimu, Serikali imekuwa ikiingia ubia na baadhi ya Shule binafsi ambazo hupokea  wanafunzi wenye uhitaji maalum, shule hizo hupamgiwa  walimu na  kupewa ruzuku ya uendeshaji hivyo Shule ya Mwalimu Tutuba ilikuwa katika mchakato wa kuingia  ubia na serikali lakini haukukamilika, hivyo Serikali baada ya  kujiridhisha mwalimu aliyepangiwa katika shule hiyo amepangiwa  katika shule ya sekondari Malagarasi.

Kwa upande wa  wahitimu waliomaliza kidato cha nne mwaka 2017, 2018 na 2019 kupangiwa vituo vya kazi Mhandisi Nyamhanga ameeleza  waombaji wa ajira walitumia  mwaka wa kuhitimu chuo badala  ya mwaka wa kuhitimu  kidato cha nne ambapo waombaji 27 waliandika mwaka 2019, waombaji 27 waliandika mwaka 2019 na waombaji 13 waliandika mwaka 2017, Serikali ilihakiki vyeti vyao  na kubaini  kuwa waombaji hao walihitimu  kidato cha nne kati ya mwaka 2010 hadi 2014.

Kwa kuongezea amesema kuwa Serikali imefuata  utaratibu wa kuhakikisha Waombaji wote waliopata nafasi ya ajira wanazingatia  vigezo vilivyotolewa  katika tangazo la ajira ambapo lilifafanua kuwa mwombaji asizidi umri wa miaka 45.

Aidha Mhandisi Nyamhanga amewalekeza  Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakiki vyeti halisi  vya waliopata ajira na kujiridhisha  kabla ya kutoa barua  za ajira, na kusisitiza kuwa endapo  itabainika  udanganyifu au kasoro za vyeti vya kitaaluma  wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimeti ya utumishi wa umma na utawala bora Dkt. Laurean Ndumbaro amesema  Serikali imetoa ajira za waalimu kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza  wametoa ajira 8000 na awamu ya pili watatoa kwa waalimu  5000  ili kupunguza malimbikizo ya mshahara kwa waalimu wapya.

Naye Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo ameweka wazi kuwa Serikali itahakikisha waalimu wote waliomba ajira kwa masomo waliyoomba yanaendana na masomo wanayoyafundisha
.

from MPEKUZI

Comments