Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi akipokea Nishani Maalum ya juu ya Mlima Kilimanjaro kutoka kwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Iringa, Baba Askofu Mstaafu Elinaza Sendoro wakati wa Mahafali ya 23 ya Chuo hicho Mjini Iringa.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi akionesha Nishani Maalum ya juu ya Mlima Kilimanjaro aliyopokea kutoka kwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Iringa, Baba Askofu Mstaafu Elinaza Sendoro wakati wa Mahafali ya 23 ya Chuo hicho Mjini Iringa.
Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Brigedia Jenerali John Julius Mbungo akionesha Nishani Maalum ya juu ya Mlima Kilimanjaro aliyopokea kutoka kwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Iringa, Baba Askofu Mstaafu Elinaza Sendoro wakati wa Mahafali ya 23 ya Chuo hicho Mjini Iringa.
…………………………
Na Kanali Juma Nkangaa SIPE, Iringa
Chuo Kikuu cha Iringa (zamani Tumaini University) kimemtunukia Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Salvatory Venance Mabeyo Nishani Maalum ya Mlima Kilimanjaro (University of Iringa Miunt Kilimanjaro Award) ambayo hutolewa kwa Viongozi wa juu Serikalini ambao wametoa mchango wa kutukuka kwa Chuo au Tasnia ya Elimu kwa ujumla. Tukio hilo limefanyika wakati wa Mahafali ya 23 ya Chuo hicho yaliyofanyika katika “campus” ya Chuo Mjini Iringa tarehe 28 Nov 20.
Mwingine aliyetunukiwa Nishani hiyo Maalum ya juu wakati wa Mahafali hiyo ni Mkurugenzi wa TAKUKURU, Brigedia jenerali John Julius Mbungo. Kwa mara ya kwanza Nishani hiyo ilitunukiwa kwa aliyekuwa Rais (Mstaafu) wa Awamu ya Tatu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Benjamin William Mkapa na Mkewe Mama Anna Mkapa wakati wa Mahafali ya 22 ya Chuo hicho mwaka 2019.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment