Takukuru Yazipongeza Halmashauri Babati Kwa Kutoa Mikopo Kwa Makundi Maalumu

MKUU wa Takukuru Mkoani Manyara, Holle Joseph Makungu amezipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Babati na Halmashauri ya Mji wa Babati, kwa kutoa mikopo ya shilingi milioni 200 isiyo na riba kwa makundi maalumu.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Babati, Makungu amesema Halmashauri hizo mbili kwa mwaka 2019/2020 zimetoa mkopo wa shilingi milioni 200 kwa makundi maalumu ya wanawake, vijana na walemavu.

Amewahimiza wananchi ili kupunguza kazi ya kushughulikia mikopo umiza wajiunge kwenye vikundi ili kupata mikopo halali inayotolewa bila riba.

Amesema kwa muda sasa wamekuwa wakishughulikia kurejesha fedha kwa wananchi waliodhulumiwa kutokana na wakopeshaji wasio na leseni kinyume cha sheria ya fedha The Microfinance Act, 2018.

Hata hivyo, ameufahamisha umma kuwa TAKUKURU wanazo taarifa kuwa wapo baadhi ya mawakala wa vyama vya kisiasa wanaochukua vitambulisho vya kupiga kura kwa kuwadanganya kuwa watawapa mikopo.

Amesema wanawake hao wanapaswa kufahamu kuwa kadi hizo zinakusanywa ili kuwanyima wao haki ya kuchagua kwa njia ya kura viongozi wanaowataka kinyume cha ibara ya (21) ya katiba ya Tanzania.

Amesema kifungu cha 16 cha sheria hiyo kimepiga marufuku kwa mtu kufanya biashara ya fedha au kutoza riba bila ya kuwa na leseni na atakayedhibitika na kosa hilo adhabu yake ni kifungo kisichopungua miaka miwili jela au faini ya shilingi milioni 20 au vyote kwa pamoja.

Amewaonya baadhi ya mawakala wa vyama vya siasa wanaokusanya kadi za kupiga kura hasa za wanawake kwa udanganyifu kuwa watawapa mikopo.

Amesema wanawake hao wanapaswa kufahamu kuwa kadi hizo zinakusanywa ili kuwanyima wao haki ya kuchagua kwa njia ya kura viongozi wanaowataka kinyume cha ibara ya (21) ya katiba ya Tanzania.

Amesema kifungu cha 16 cha sheria hiyo kimepiga marufuku kwa mtu kufanya biashara ya fedha au kutoza riba bila ya kuwa na leseni na atakayedhibitika na kosa hilo adhabu yake ni kifungo kisichopungua miaka miwili jela au faini ya shilingi milioni 20 au vyote kwa pamoja.

"Kwa wale ambao kadi zao za kupigia kura zimechukuliwa na walaghai hao, pia wale ambao kwa bahati mbaya wamepoteza kadi hizo ili kurejesha haki hiyo ya kikatiba Tume ya uchaguzi imeshatoa utaratibu ambao kitambulisho cha Taifa na leseni ya udereva itatumika," amesema Makungu.

from MPEKUZI

Comments