Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi kisiwani Zanzibar limesema limelazimika kutumia mabomu ya machozi katika baadhi ya maeneo kutokana na uwepo wa viashiria vya uvunjifu wa amani.
Limesema waliokamatwa ni waliochoma matairi na kuyaweka katikati ya barabara na waliokwenda katika vituo vya kupigia kura wakati leo wanaoruhusiwa kupiga kura ni makundi maalum wakiwemo askari wa vikosi vya ulinzi na usalama pamoja na kuyashambulia kwa mawe magari ya polisi.
Hayo yameelezwa leo Jumanne Oktoba 27, 2020 na Kamanda Polisi wa Mkoa huo, Awadh Juma Haji
Amesema mbali ya matumizi ya mabomu hayo, wanawashikilia baadhi ya vijana waliodai kuhusika katika matukio hayo.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment