Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, John Magufuli amesema kilichomtokea Waziri Mkuu wa zamani Fredrick Sumaye hadi kuhamia upinzani ni mapepo lakini sasa roho mtakatifu amemuokoa.
Akizungumza kwenye mkutano wa kampeni mjini Babati Jumapili Oktoba 25, Magufuli amesema “Sumaye ni mwana CCM halisi aliyepotea kwa bahati mbaya kutokana na mapepo yaliyomkumba siku za nyuma.
“Nakushukuru sana umefanya uamuzi mzuri. Huyu alikuwa waziri mkuu nikiwa waziri wake. Kama ilivyo kawaida Mungu alipoumba malaika wengine wakagoma wakatupwa duniani, wale ndio wakamgusa Mzee Sumaye miaka kadhaa akahamia chama ambacho ni cha ajabu.
Bahati nzuri Mzee huyu alijifunza mapema akawakimbia amerudi CCM karibu sana baba. Sumaye ni mwadilifu, hicho chama hakikumfaa, chama kinachosimama hadharani na kumtukana kila mmoja, chama kisichokuwa na staha.”
Amesema,” Ninamshukuru roho mtakatifu aliyekugusa Mzee Sumaye na ukarudi nyumbani, kufanya kosa si kosa kurudia kosa ndio kosa. Ninajua umefika nyumbani hongera Mungu akubariki na uzao wako,” amesema Magufuli.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment