Fatma Karume Afutwa Uwakili

Kamati ya Maadili ya Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), imeondoa moja kwa moja jina la Fatma Karume katika orodha ya mawakili baada ya kumkuta na hatia ya kukiuka maadili ya uwakili.

Kwa uamuzi huo, Fatma mwenye namba ya uwakili 848 hataruhusiwa kufanya kazi za uwakili ndani ya mipaka ya Tanzania Bara mpaka itakavyoamriwa vinginevyo.

Baada ya uamuzi huo kutolewa mapema jana, Fatma ambaye ni mtoto wa Rais mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume, aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba hatakata rufani kupinga uamuzi huo.
 
Kung’olewa kwa Fatma TLS kunakuja ikiwa ni siku kadhaa zimepita  tangu Kampuni ya Uanasheria ya IMMMA aliyoshiriki kuianzisha kumfukuza kazi.

Barua ya Kampuni ya IMMMA ya tarehe 16 Septemba 2020 iliyosainiwa na Sadock Magai, Mkurugenzi Mwenza wa kampuni hiyo ilisema, Fatma ameondolewa katika sehemu ya umiliki wa kampuni baada ya mkabata wake alioingia tarehe 26 Machi 2007 kuvunjwa.



from MPEKUZI

Comments