Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imetoa zaidi ya shilingi bilioni 15 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa miradi mbalimbali ya miundombinu ya kutoa huduma kwa jamii katika Wilaya ya Buhigwe, Kasulu Mjini, Kasulu Vijijini na Kibondo mkoani Kigoma.
Hayo yamesemwa na na Meneja wa TANROADS Mkoa wa Kigoma, Mhandisi Narcis Choma alipokuwa akitoa taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya mtandao wa barabara ya Afrika Mashariki (EARNP) inayojenga mkoani humo.
Choma amesema kuwa AfDB imetoa mkopo nafuu wa Dola za Marekani milioni 256.2 kwa ajili ya kujenga barabara ya kujenga barabara ya kutoka Kabingo-Kasulu hadi Manyovu yenye urefu wa 260km. Ujenzi wa barabara hiyo ni moja ya utekelezaji wa miradi ya EARNP ambao unaiunganisha Tanzana na Burundi.
Kutokana na fedha zilizotolewa na benki hiyo miradi mbalimbali itatekelezwa katika wilaya hizo ikiwa ni pamoja na vituo vya mabasi, shule za msingi na sekondari, ujenzi wa masoko na ukarabati wa mabomba ya kusambaza maji, ujenzi wa vituo ya afya na hospitali za wilaya pamoja na barabara za mtaa.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment