Shule ya Mivumoni Islamic Yaungua kwa Mara ya 3

Shule ya Sekondari ya Mivumoni Islamic, iliyopo katika eneo la Msikiti wa Mtambani Kinondoni Dar es Salaam, imeteketea kwa moto Alafajiri ya leo Agosti 31, 2020, na kuelezwa kuwa hii ni mara ya tatu shule hiyo kuungua ndani ya kipindi cha miezi miwili.

Kamishina Msaidizi Mwanadamizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kinondoni Salum Mohamed, amesema kuwa taarifa ya chanzo cha moto huo itatolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Aboubakar Kunenge.

"Kwa kipindi cha miezi miwili hili ni tukio la tatu katika shule hii, Julai 18 tulipata tukio la moto la muundo huu na tulizima, Julai 23 tukio la moto tena lilitokea hili ni tukio la tatu mfululizo ndani ya eneo moja, ni matukio ambayo yanaendelea kutokea ndani ya hizi Shule za Kiislamu za Jijini Dar es Salaam, uchunguzi umefanyika na Msemaji wa hili ili kujua chanzo ni nini ataitoa Mkuu wa Mkoa " amesema Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto.


from MPEKUZI

Comments