Watu watano wamefariki dunia papo hapo katika ajali ya barabarani kijijini Nyasamba, wilayani Kishapu mkoani Shinyanga.
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba amesema chanzo cha ajali hiyo ni gari dogo kupoteza mwelekeo na kugonga basi dogo lililokuwa likitokea Mwanza kuelekea mkoani Tabora.
“Gari lenye namba za usajili T571 BPZ aina ya Tata Mini Bus ikiendeshwa na Kazimili Maganga likitokea Mwanza kwenda Tabora lilipofika eneo la Nyasamba liligongana na gari jingine dogo likitokea Dar es salaam likiendeshwa na Ramadhan Silaji na kusababisha vifo vya watu watano
“Chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa madereva wa magari yote mawili na uzembe wa dereva dogo ambapo alihama upande wa kushoto na kuendeshea kulia zaidi na kwenda kugongana na basi hilo dogo na kusababisha vifo vya watu watano” Amesema Kamanda Magiligimba

from MPEKUZI
Comments
Post a Comment