Waziri Mkuu Kassim Majaliwa jana (Ijumaa Julai 24, 2020) alimjulia hali kijana Deogratias Mianga mkazi wa Singida ambaye amelazwa katika Taasisi ya tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI) kwa ajili ya matibabu.
Waziri Mkuu alimuona Deogratias kupitia vyombo vya habari akiomba msaada wa matibabu kutokana na matatizo ya mgongo. Waziri Mkuu aliguswa na hali ya Deogratius na tarehe 02/07/2020 alimuwezesha kufika MOI na kufanyiwa upasuaji tarehe 06/07/2020.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment