Namna ya kutuma pesa kutoka Kenya, Uganda na Rwanda kwa mteja wa Tigo Pesa


Kampuni inayoongoza katika kuhakikisha mtanzania anaishi Maisha ya kidijitali,Tigo Tanzania, imeweza kurahisisha utumaji na upokeaji wa pesa, Huduma hii ni wazi sasa kwamba inawaunganisha wateja wa Tigo Pesa na mitandao mingine mikubwa ya mawasiliano katika ukanda wa Afrika Mashariki inayotoa huduma za kifedha kupitia simu za mkononi hatua ambayo itakuza wigo wa kufanya miamala ya kifedha bila kujali mipaka baina ya nchi moja na nyingine.
 
Mteja ataweza kutuma fedha kupitia maelekezo yaliopo hapa chini;
 
Kenya - Safaricom
Menu ya *840#
Piga *840# 1. Kubali Vigezo na Masharti Kisha 1.Chagua kutuma Pesa Nje ya Nchi Kisha 1.Tuma kwa namba ya Simu Kisha Ingiza Namba ya Simu ya mpokeaji kwa mfumo wa Kimataifa (255xxxxx).
Ingiza Kiasi kwa Fedha ya Kenya (KES) Kisha Chagua Chanzo cha Mapato Kisha Chagua sababu za kutuma pesa Kisha 1. Kubali na ingiza Namba ya Siri.
MySafaricom App Nenda kwenye Application yako ya MySafaricom App-Chagua M-PESA - Chagua M-PESA Global - Kubali Vigezo na Masharti - Chagua Kutuma Pesa kwenda Namba ya Simu-Chagua Nchi - Ingiza namba ya Simu: Kiasi kwa Shilingi ya Kenya (KES) - Chagua chanzo cha mapato-Hakikisha kwa kuingiza Namba Siri.

Rwanda - MTN Rwanda
Menu ya *182#
Piga *182# - 1.Tuma Pesa - 2.Kwenda nchi nyingine - 4.Tanzania - Ingiza Namba ya mpokeaji kwa kutumia Mfumo wa Kimataifa (255xxxxx) - Ingiza Kiasi (Shilingi ya Rwanda) - 1.Kubali kuthibitisha Muamala.
Rwanda - Airtel Rwanda
Menu ya *500#
Piga *500# - 1.Tuma Pesa - 3.Kimataifa - 1Tanzania - 1.Tigo Pesa - 1.Tuma -  Ingiza Namba kwa mfumo wa kawaida (0713xxxxxxx) - Ingiza Kiasi - Weka namba ya Siri.
 
Uganda - MTN Uganda
Menu ya *165#
Piga *165# - Chagua “Kutuma Pesa” - Chagua Afrika Mashariki - Chagua Tanzania - Chagua Tigo Tanzania - Ingiza namba ya Mpokeaji (Anza na +255)-Ingiza Kiasi (Pesa ya Uganda) - Ingiza namba ya Siri kuthibitisha muamala.
 
Huduma hii ni muendelezo wa ari ya Tigo Tanzania kuelimisha mteja jinsi ya kuipata huduma hii akiwa nchini kwake.


Mwisho.



from MPEKUZI

Comments