Msemaji wa familia aeleza sababu za kifo cha Mzee Mkapa

Siku tatu za kuuaga mwili wa Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa zimeanza rasmi leo katika Uwanja wa Uhuru, Dar es salaam.

Zoezi hili la kuuaga mwili wa marehemu Mkapa limeanza kwa misa takatifu na litaendelea hadi Jumanne tarehe 28 Julai 2020.

Aidha, msemaji wa familia, William Erio ameeleza kuwa Hayati Mkapa alifariki dunia kutokana na mshituko wa moyo.
 
“Mzee wetu aliugua akaenda hospitali akachukuliwa vipimo akakutwa na malaria akalazwa, Alhamis mchana alikuwa vizuri, alikuwa anatazama taarifa ya habari, baada ya hapo aliinuka akataka kutoka akainamisha kichwa, mpaka walipo mpima alikua kaishafariki.

“Nilidhani ni vizuri tuliseme kwa sababu kumeanza kuwa na maneno maneno kwenye mitandao, niwaombe na kuwasihi Watanzania wenzangu tumuenzi Mzee wetu aliyetangulia mbele ya haki kwa kuheshimu ukweli huo, kwamba hicho ndicho kilichosababisha kifo chake” Mwanafamilia ya Mkapa

Mwili wa Mzee Mkapa umehifadhiwa katika eneo maalum tayari kwa wananchi kutoa heshima za mwisho.


from MPEKUZI

Comments