Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa amesema kuwa maandalizi ya mazishi ya Rais Mstaafu, Benjamin Mkapa yamekamilika kwa zaidi ya asilimia 50.
Akizungumza na TBC katika Ikulu ndogo ya Mtwara, Byakanwa ameeleza kuwa wameandaa utaratibu wa usafiri wa kutoka Masasi kwenda kijijini Lupaso kwenye mazishi ili kuepusha kila mtu kutumia gari lake kufika huko.
Hata hivyo amesema kuwa utaratibu huo hautazuia watu kwenda na magari yao, lakini lengo lao ni kupunguza idadi ya magari yanayokwenda huko ili kuruhusu watu wengi zaidi kukusanyika.
Aidha, amesema serikali ya mkoa imeandaa utaratibu wa maeneo ya malazi kwa watu watakaokuja katika mazishi ya Rais Mstaafu, na amewahakikishia wote usalama wa kutosha katika kipindi chote watakachokuwa mkoani hapa.
Credit: TBC
Credit: TBC
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment