New Victoria Hapa Kazi Tu Kumaliza Changamoto ya Usafiri Kagera-Mwanza....Gaguti Asema Itatua Bandari Ya Bukoba Juni 28 Mwaka Huu.

Na Avitus Benedicto Kyaruzi, Kagera.
Wananchi Mkoani Kagera wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika mapokezi ya Meli ya New Victoria Hapa Kazi tu  kwenye bandari ya Bukoba ikiwa ni sehemu ya majaribio ya meli hiyo ambayo ilikuwa kwenye matengenezo jijini Mwanza. 
 
Hayo yameelezwa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti  wakati akiongea na waandishi wa habari mnamo tarehe 26 juni 2020 ofisini kwake na kuwataka wananchi wa mkoa huo kujitokeza kwa wingi katika mapokezi ya meli iyo kutoka bandari ya mwanza South kuja katika bandari ya Bukoba. 
 
Gaguti Amema kuwa meli hiyo ipo katika safari yake ya  majaribio baada ya kukamilika kwa ukarabati mkubwa na kusema kuwa meli hiyo itatua katika bandari ya Bukoba mnao tarehe 28 juni 2020 siku ya Jumapili majira ya saa nane mchana.

Ikumbukwe kuwa meli hii iliwahi kufanya kazi kwa kipindi cha nyuma kwa muda mrefu na baada ya hapo ikatakiwa kufanyiwa marekebisho makubwa ambayo mpaka sasa yamekamilika. 
 
Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa baada ya kutua bandarini wananchi watapata fursa ya kuiombea dua meli hiyo na kuibariki ili iweze kuanza kutoa huduma katika siku za hivi karibuni katika ziwa Victoria na kuanza upya amshaamsha ya kiuchumi ya mji wa Bukoba na mkoa wa Kagera kwa ujumla.
 
Ameongeza kuwa katika safari hiyo ya majaribio hakutakuwa na abiria lakini Mh  Rais John Pombe Magufuli ameridhia katika safari hii ya majaribio wananchi wa Mkoa huo watapata fursa ya kusafirisha mizigo yao zaidi tani 100 kwenda Mwanza bure ikiwa ni kuamsha, kuchagiza na kukumbusha kuwa meli hii tofauti na kusafirisha abiria ilikuwa kiungo kikubwa cha usafirishaji wa bidhaa kutoka Mwanza –Bukoba na Bukoba-Mwanza.


from MPEKUZI

Comments