Naibu Waziri Masauni: - Changamoto Makazi Ya Askari Kuwa Historia

Serikali iko mbioni kumaliza changamoto za makazi ya Askari nchi nzima ikiwa ni mkakati wa Uongozi wa  Awamu  ya  Tano  kutatua changamoto hiyo iliyodumu kwa muda mrefu katika vyombo vilivyopo ndani ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ikiwemo Jeshi la Polisi, Magereza, Zimamoto na Uhamiaji.

Hayo yamesemwa  Visiwani  Pemba  na  Naibu  Waziri  wa  Mambo ya Ndani  ya  Nchi, Mhandisi  Hamad  Masauni  baada  ya  kukagua nyumba 14  kati  ya nyumba  400 zilizopo katika hatua mbalimbali za ukamilishwaji na nyingine zushakamilika  huku  gharama  za ujenzi  wa nyumba  hizo  ni  Bilioni 10 zilizotolewa  na  Rais  wa      Jamhuri ya Muungano, Dkt. John Pombe Magufuli, mwezi  April, 2018 mkoani Arusha wakati wa Kumbukumbu ya Hayati Abeid Amani Karume.

“Serikali ya Awamu ya Tano  imekua  inatambua changamoto za makazi ya askari na ujenzi wa nyumba hizo 400 ulishaanza nchi nzima na nyingine zishakamilika, napenda kuwaahidi askari wetu changamoto hiyo ya makazi itakua historia ndani ya muda mfupi, nimetembea baadhi ya mikoa nimeona jinsi askari wetu wanavyoishi.”alisema Masauni

“…lakini baadhi ya mikoa tushajenga nyumba ikiwemo nyumba za askari  magereza  Ukonga, nyumba za uhamiaji Iyumbu Dodoma, nyumba za polisi Medeli, Dodoma na mikoa yote nchini kuna nyumba ambazo askari wetu washaanza kukaa” aliongeza Masauni

Wakizungumza baadhi ya askari wanaokaa katika nyumba hizo za Pemba waliishukuru serikali kwa kuwajengea makazi ambayo yamepunguza changamoto hiyo huku wakiweka wazi ilikua ngumu kuchanganyika na raia mtaani lakini sasa wanaamini makazi hayo yatawafanya wafanye kazi zao kwa umakini na uadilifu mkubwa.

Mradi huo wa nyumba zilizopo katika eneo la Mfikiwa ChakeChake Kusini Pemba umekamilika na unajumuisha nyumba 14 ambapo jumla ya familia 14 za askari polisi zinatumia makazi hayo.


from MPEKUZI

Comments