Mufti Mkuu Tanzania Asema hakutokuwa na ibada ya Hijja Mwaka huu

Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Abubakar Zubeir bin Ally kwa niaba ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), ametangaza kuwa mwaka huu hakutokuwa na ibada ya hijja hii ni kutokana na kauli iliyotolewa wiki hii na serikali ya Saudi Arabia kutokana na janga la Corona.

Abubakar Zubeir bin Ally ameyasema hayo leo Juni 25, 2020 wakati akiongea na waandishi wa habari ambapo ameeleza kuwa janga la Corona ndio limesababisha na haitakuwa kwa Tanzania pekee tu bali kwa Dunia nzima isipokuwa waislam waliopo ndani ya Saudi Arabia.

Ameeleza kuwa BAKWATA wameunga mkono maamuzi hayo ya Saudi Arabia lengo likiwa ni kuweka usalama kwa waumini na kuwakinga na Corona kwasababu ugonjwa huo ni wa kuambukiza.

Aidha, Mufti Zubeir amezitaka madrasa zote nchini kuanzia sasa kurejesha shughuli zote za madrasa nchini huku zikizingatia taratibu zote za kiafya kama inavyoshauriwa na wataalamu wa afya nchini.


from MPEKUZI

Comments