Idadi ya maambukizi ya virusi vya Corona nchini kenya imefikia watu 1962 hii ni baada ya watu 74 kuthibitishwa kuwa na virusi hivyo katika muda wa saa 24 zilizopita.
Kaunti za Nairobi na Mombasa zimeendelea kushuhudia idadi kubwa ya maambukizi,Nairobi ikisajili maambukizi 35 na Mombasa 23.
Idadi ya waliofariki imefikia 64 baada ya mtu mmoja zaidi kufariki, aidha waliopona wamefikia 474 baada ya watu 14 zaidi kupona na kuondoka hospitalini.
from MPEKUZI
Comments
Post a Comment