Riwaya Kali ya Kusisimua....SIN- Sehemu Ya Saba (07)

Mwandishi- EDDAZARIA G.MSULWA
Age-18+
Simu-0657072588(whatsapp) au 0768516188


ILIPOISHIA   
“Yaani sijui kwa nini uliaolewa na yule mzee”
“Ahaa ni maisha tu. Tumefika baba yangu”
Mrs Sanga alizungumza huku akisimamisha gari lake nyuma ya gari la Tomas alilo liacha kwenye maegesho ya ofisi za rafiki yake.
“Haya shuka, acha mimi niwahi nyumbani”
“Sawa mke wangu”
Tomas taratibu akafungua mlango wa gari la mrs Sanga na kushuka huku akiwa na mfuko wenye pesa. Mpelelezi mmoja akaanza kazi ya kumpiga picha Tomas bila ya yeye kufahamu. Huku mpelelezi mwengine akitoa ripoti kwa mkuu wao kwamba wamempata jambazi aliye mteka nabii Sanga.


ENDELEA
“Hakikisheni kwamba hamumpotezi mtuhumiwa”
“Sawa mkuu”
“Pia kuweni makini kumfatilia na ikiwezekana muweze kumkamata hata kabla hajafanya jambo lolote”
“Sawa sasa mkuu”
Tomas pasipo kujua chochote akaingia kwenye gari lake aina ya Toyota Prado Tx. Tomas akaanza kuondoka eneo hilo huku akiwa na furaha ya kujivunia milioni ishirini za bure, kwani makubaliano yake na watekaji ni kuwalipa milioni arobaini.
                                ***
“Mage Mkinga una ndugu?”
Sheby aliuliza huku akipunguza mwendo, kwani mbele yao kuna tuta refu kidogo.
“Hapana”
“Au unakwenda kwa shemeji?”
“Hakuna kitu kama hicho Sheby”
“Ila nini tena jamani?”
“Kuna mambo yangu nakwenda kuyafanya”
“Mmmmm….ila unaweza kunipa nafasi ya kuzungumza”
“Kuzungumza nini?”
“Ahaa….katika siku zote za maisha yangu, nimetokea kukupenda Mage, ila nilikuwa nina tafuta muda muafaka wa kuweza kukueleza hilo”
“Ila Sheby wewe si unaishi na mwanamke?”
“Ndio nina ishi naye tu, ila ukweli ni kwamba sina mapenzi naye”
“Acha uongo Sheby na yule dada alivyo mzuri, inakuwaje huna mapenzi naye?”
“Unaweza kuishi na mtu ila usimpende. Hivyo ni sawa na mimi, nina ishi naye tu ila ukweli ni kwamba simpendi”
“Inakuwaje una ishi na mwamke usiye mpenda?”
“Ana mimba yangu na hicho ndio kinacho mfanya kuwepo kwangu. Ila ingekuwa sio mimba wala nisinge kuwa naye”
“Sheby muogope Mungu.  Mpende mtoto wa watu usije ukamuumiza kwa chochote”
“Ila simpendi?”
“Sawa humpendi na mbaya ana kwenda kuwa mama wa mwanao. Hivyo mpende na kumuheshimu bwana”
“Haya bwana. Ila hata siku moja sijawahi kumuona shemeji yetu. Vipi?”
“Usijali utamuona”
“Ni nani?”
“Ahhaa….wewe si unataka kumuona. Utamuona siku itakapo fika”
“Haya bwana”
Safari ikazidi kusonga huku wakizungumza mambo mengi sana kuhusiana na maisha. Majira ya saa moja kasoro wakafika Mkinga. Magreth akatoa simu  yake na kupiga namba ya watekaji.
“Nimefika Mkinga”
“Upo na nani?”
“Dereva taksi”
“Muache hapo stendi na panda pikipiki na umpatie simu dereva wa pikipiki nitampatia maelekezo ya wapi anapaswa kukuleta”
“Sawa”
Simu ikakatwa.
“Nani huyo”
“Ni jamaa yangu. Ameniambia nikuache hapa kwa maana huko ninapo kwenda gari haiwezi kuingia. Nitapanda pikipiki, kisha nitapelekewa huko ninapo pahitaji”
“Sawa, kwa hiyo nikusubirie hapa kwa muda gani?”
“Hadi nitakapo rudi. Nipatie namba yako ya simu”
Sheby akamtajia Magreth namba yake ya simu. Magreth akashuka kwenye taksi hiyo. Waendesha pikipiki kama kawaida yao ya kumkimbilia mteja, ndivyo jinsi walivyo fanya kwa Magreth. Magreth akamchagua dereva mmoja kati ya watano walio mfata. Akapiga simu kwa watekeji.
“Mpatie dereva pikipiki simu”
Magreth akampatia dereva pikipiki simu. Baada ya kuelekezwa wapi ampeleke Magreth simu hiyo ikakatwa.
“Una pafahamu?”
“Ndio”
“Itakuwa kiasi gani?”
“Elfu kumi”
“Ni mbali sana?”
“Sio sana”
“Haya”
Magreth akapanda pikipiki na kuondoka eneo hilo la stendi. Ndani ya dakika arobaini na tano, wakafanikiwa kufika karibu kabisa na msitu huo. Magreth akashuka na kumlipa na dereva pikipiki akaondoka. Simu ya Magreth ikaita na kuipokea. Tembea hatua kumi mbele kisha kunja kushoto utaona gari nyeusi”
Magreth akaanza kutembea huku simu yake ikiwa sikioni mwake. Baada ya hatua hizo kumi akakunja kushoto na kuona gari nyeusi ikiwa imefichwa vichakani. Japo kigiza kimeanza kuingia ila hakuweza kuogopo kwa lolote kwani tayari amesha dhamiria kumuokoa nabii Sanga. Wanaume wawili walio zifunika sura zao wakatoka ndani ya gari hilo huku wakiwa na bastola mikononi mwao.
“Vua begi”   
Magreth akavua beigi hilo mgongoni na kulishika mkono wa kulia. Watekeji hao wakaanza kumpapasa mwili wake wote. Walipo hakikisha hana silaha wala kinasa sauti wakaichukua simu yake kisha wakamfunga kitambaa cheusi usoni mwake. Wakamuingiza ndani ya gari, ili kumchanganya Magreth asitambue ni wapi anapo elekea, wakaanza safari ya kurudi mjini. Walipo karibia na mjini, wakageuza gari na kuianza safari ya kurudi msituni huku gari hilo likiendeshwa kwa kasi sana. Wakafika msituni, wakamshusha Magreth kwenye gari, wakaongozana naye hadi kwenye chumba walipo muweka nabii Sanga.
                                ***

Wapelelezi hawa wakazidi kulifaafilia gari la Tomas kwa umakini sana. Tomas akatoa simu yake mfukoni, akatafuta namba ya Rama D, ambaye ndio kiongozi mkuu wa kikosi cha watekaji hao.
“Mzee baba”
“Niambie mwana”
“Vipi huyo boya ana endeleaje?”
“Yupo fresh, ana mbwela mbewle tu hapa”
“Chok** huyo. Sasa ni hivi mzee baba. Ninawaletea mpunga wenu muda huu”
“Muda huu?”
“Ndio”
“Fresh mwana, ni wewe ila kuwa makini”
“Usijali mwana nipo makini sana. Ila hakikisheni kwamba hamumpigi kwa maana bibie ana mbwela kishenzi”
“Ahahaa”
“Yaa nyinyi hakikisheni kwamba ana kuwa salama huyo mzee”
“Poa poa mwana, hilo halina tabu, kikubwa mpunga uwe mezani”
”Fresh mida”
“Poa”
Kitendo cha Tomas kukata simu, akastukia gari ndogo ikimpita kwa kasi na kupunguza mwendo hadi ikamlazimu na yeye kupunguza mwendo.
“Huyu msen** nini, anapunguzaje mwendo?”
Tomas alizungumza kwa hasira huku akipiga honi. Dereva wa gari hilo akaligeuza gari lake na kulifanya liifunge barabara nzima. Tomas akasimamisha gari lake na kushuka kwa hasira sana huku akimfaata dereva wa gari hilo.
“Wewe msen** umelewa nini?”
Tomas aliporomosha matusi. Wapelelezi hao wakashuka kwenye gari lao huku wakichomoa bastola zao. Kitendo hicho kikaanza kumtetemesha Tomas.
“Ka…kaaakkk…..ma…..”
Mpelelezi mmoja hakumpa nafasi Tomas ya kumalizia sentensi yake. Akampiga mtama mmoja matata na kumfanya arushwe juu kimo cha mbuzi na kuanguka mzima zima. Mpelelezi huyo akamgeuza Tomas na kumlaza kifudifudi. Akamuwekea kigoti cha shingoni huku akiichomeka bastola yake kiunoni mwake na kutoa pingu mfukoni mwake. Akaifunga mikono yake hiyo na kumnyanyua. Kitendo hicho kikamfanya Tomas atambue kwamba watu hao ni polisi na si majambazi kama alivyo hisi kwa mara ya kwanza.
“Munanikamata nini? Kosa langu ni nini?”
“Ushibitisho wa pesa upo hapa”
Mpelelezi ambaye alikuwa akikagua gari la Tomas alizungumza huku akitoa mfuko huo wenye milioni arobaini.
“Poa piga picha ushahidi kisha endesha gari lake na mimi nina muingiza huku. Una haki ya kukaa kimya, kila kitu utakwenda kukijua kituoni”
Mpelelezi huyo alizungumza huku akimuingiza Tomas, ndani ya buti ya Alteza na kuifunga. Akaingia ndani ya gari hilo, kisha wakageuza na kuanza safari ya kuelekea central Polisi.
                                ***
    Magreth akafunguliwa kitambaa alicho fungwa usoni mwake. Macho yake yakakutana na nabii Sanga, aliye kaa kwenye kiti huku pembeni yake wakiwa wamesimama watu wa wiwili wenye mitutu ya bunduki aina ya AK47. Akataka kumkimbilia na kumkumbatia, ila mtekaji mmoja akamzuia.
“Tunahitaji kuziona pesa”
Magreth akaliweka chini begi hilo na kulifungua. Vitita vya dola za Kimarekani, vikawafanya watekaji hao wawili walio kuwa karibu na begi hilo kutazamana. Kwa isharaha mkuu wao akamuagiza mmoja wao kuzimwaga pesa hizo juu ya meza. Vibunda hivyo vikamwagwa juu ya meza  na kuifanya mioyo ya watekaji hao kujawa na furaha.
“Kalete mashine”
“Sawa”
Mtekaji mmoja akatoka, baada ya dakika mbili akarudi akiwa na mashine ya kuheshabia pesa. Wakaanza kazi ya kuhesabu vibunda hivyo vya pesa. Ilipo timia dola elfu sitini, mkuu wao akampa mkono wa kumshukuru nabii Sanga.
“Unaweza kuzungumza chochote mzee”
“Ni nani ambaye amewapa oda ya kuniteka?”
“Ni kutoka kwa kijana wako Tomas ambaye ni dalali wako”
“Tomas?”
“Ndio na hapa ninavyo zungumza yupo njiani ana ileta milioni ishirini kwa ajili ya kazi tuliyo mfanyia.”
Nabii Sanga akakaa kimya huku akiisikilizia hasira jinsi inavyo utafuna moyo wake. Akanyanyuka kwenye kiti hicho huku macho yakitawaliwa na uwekundu. Muda wote Magreth yupo kimya akishuhudia jinsi nabii Sanga alivyo kasirishwa kwa kitendo hicho kibaya alicho fanyiwa.
“Ana kuja hapa eheee?”
“Ndio mzee”
“Sasa hiyo ni milioni mia na ishirini. Hizi ishirini anazo zileta chukueni na hiyo ishirini ya ziada aliyo zidi, hakikisheni muna mchinja mume nielewa?”
Kauli ya nabii Sanga ika mstua sana Magreth, ila hakuweza kufungua kinywa chake kwa maana hajajua ni makubaliano gani nabii Sanga ameingia na watekaji hao.
“Sawa mkuu”
“Tena nina hitaji mumkate kate kiungo kimoja baada ya kingingine na mumuambie kwamba mimi ndio nimetoa kazi hiyo”
“Sawa mzee”
“Na kuanzia hivi sasa, nitakuwa nina wapa kazi zangu. Nahitaji muzifanye kwa uhakika na sitaki kabisa mulegelege, kama muna taka pesa zaidi ya hii basi mushikamane na mimi sawa”
“Sawa, ila tunahitaji kukudhibitisha kwamba huto tusaliti. Wote hapa tumeingia kiapo cha damu hivyo na wewe tuna hitaji uingie kiapo cha damu”
“Hilo halina shida. Niambieni nifanye nini?”
Mmoja wao akatoa kisu. Wakamtazama Magreth, wakampa ishara ya kutoka ndani humo na Magreth akatii. Wakaufunga mlango wa chumba hicho. Wakavua vinyago vilivyo ficha sura zao.
“Mimi ninaitwa Rama D. Sisi sote ni watoto wa familia moja na mimi ndio kaka yao. Huyu anaitwa Selemani D. Huyu anaitwa Rashid D na huyu ni mdogo wetu wa mwisho ana itwa Abdalah D. Baba yetu alikuwa ni komandoo wa jeshi la nchi hii. Alitupa mafunzo toka tukiwa wadogo na tumekuwa ni professional wa mbinu za kijeshi. Tuna uwezo wa kufanya kila aina ya tukio hivyo karibu katika familia”
Rama D, alizungumza huku akimtazama nabii Sanga. Nabii Sanga alipo hakikisha kwamba amewakremisha sura zao vijana hao. Akajikata sehemu ndogo ya kiganja chake na akapewa kikopo cha kuiweka damu hiyo inayo mchuruzika kiganjani. Rama D na wadogo zake wakajikata na wao na damu zao wakaziweka katika kikopo hicho, ikiwa ni ishara ya muungano wa damu.
“Nimekaribia. Nina juana na watu wengi sana duniani. Nitahakikisha nina wawezesha kisilaha, kifedha na kila aina ya mbinu mpya nitawapatia kwa maana, hadi leo hii nimekuwa tajiri si kwamba ni Mungu amenibariki, ila nilitumia kila aina ya njia kuwa tajiri. Hivyo natambua shida kama hizi”
“Karibu sana.”
Baada ya nabii Sanga kukaribishwa katika familia hiyo. Rama D na wadogo zake, wakavaa vinyango vyao. Wakafungua mlango na kumuita Magreth ndani.
“Simu yako”
Selemani D, alizungumza huku akimkabidhi Magreth simu yake.
“Huyu mwanamke nina imani wote mume muona”
“Ndio”
“Hakikisheni kwamba hakuna anaye msogelea na kila anaye jaribu kumsogelea basi mnajua nini mna paswa kufanya”
“Tumekuelewa.”
Kutokana na Magreth sio mwana familia wao. Wakamfunga kitambaa machoni mwake, kisha wakainza safari ya kuelekea Mkinga mjini huku wakiwa pamoja na nabii Sanga ndani ya gari lao.
                                ***
    Tomas akatolewa ndani ya buti ya gari hilo. Kwa mwendo wa haraka, akaingizwa kwenye kituo hicho kikubwa cha polisi. Umaarufu wake wa udalali katika jiji hilo la Dar es Saalam, likawafanya baadhi ya askari kushangaa juu ya uwepo wake hapo kituoni. Ila kutokana  ameletwa na pingu mikononi mwao hapakuwa na hata mmoja aliye wazuia wapelelezi hao kumpeleka katika chumba cha mateso. Thomas akavuliwa nguo zake zote, akafunguliwa pingu za mikononi mwake na kufungwa minyororo mizito. Akaning’inizwa hewani huku mikono yake ikiwa imechanuliwa mithili ya Yesu alivyo sulubiwa msalabani. Wapelelezi hao wakamwagia maji mwilini mwake, kisha mmoja wao ahachukua nyaya mbili za umeme, zenye hasi na chanya. Akazigusanisha na zikaanza kutoa cheche cheche, zilizo mfanya Thomas kujawa na mshangao hata kabla ya kupachikwa na nyaya hizo mwilini.
“Ukijibu kwa usahihi basi adhabu hii huto ipata. Ila ukijibu kwa jeuri basi adhabu hii utakumbana nayo.”
Kauli ya mpelelezi ikamfanya Tomas macho kumtoka huku akiwa haelewi ni kosa gani lililo mfanya kukumbana na shurba zote hizo.
“YUPO WAPI NABII SANGA”
Mapigo ya moyo ya Tomas yakaanza kumdunda kwa kasi sana kwani hakutarajia kwamba, mpango wa siri alio upanga yeye na mrs Sanga utajulikana kirahisi namna hiyo.


 ITAENDELEA
Haya sasa nabii SANGA yupo huru na ametambua kwamba Tomas ndio muhusika wa kutekwa kake. Tomas yupo mikononi mwa polisi. Je akibanwa atafichua siri nzito ambayo hata polisi wakielezwa hawato iamini?. Nini kitatokea? Endelea kufaatilia kisa hiki cha kusisimua, usikose sehemu ya 08

 


from MPEKUZI

Comments