Riwaya Kali ya Kusisimua....SIN- Sehemu Ya Tatu (03)

Mwandishi- EDDAZARIA G.MSULWA
Age-18+
Simu-0768516188

ILIPOISHIA
“Mage hivi una mchumba kwa maana sijawahi kusikia fununu pale kanisani kama kuna mchumba wako?”
Magreth akatabasamu huku akimtazama nabii Sanga kwa uso ulio jaa aibu aibu kidogo.
“Hapana baba mchungaji. Nina endelea kuulinda usichana wangu hadi pale Mungu atakapo nipatia mume wa kwangu peke yangu”
“Unataka kusema wewe bado hujawahi kutana kimwili na mwanaume?”
“Ndio baba mchungaji, bado mimi ni bikra”
Kauli hiyo ikaulipua moyo wa nabii Sanga, kwa umri wake wa miaka arobaini na sita hadi sasa, hajafanikiwa kukutana na mwanamke bikra na siku zote alikuwa akitamani sana kupata binti ambaye ni bikra kwani hata mke wake aliye muoa hakumkuta akiwa bikra


ENDELEA
“Safi sana mwanangu. Unajua vijana wa siku hizi maisha yao wameyafanya kuwa ni mabaya sana. Utakuta mabinti wenye usichana wao kwa hapa tu Dar es Salaam, hawazidi hata elfu moja. Ila wengi wao wanadumbukia kwenye mahusiano wakiwa bado ni wadogo sana”
“Ni kweli baba. Marehemu mama yangu alijitahidi sana kunilea kwenye mazingira ya dini sana. Alinichunga na kunifundisha yaliyo mema na bora. Hadi sasa nina mshukuru kwa malezi yake”
“Kweli mshukuru kwa hilo.”
Nabii Sanga alizungumza huku akiyatupia macho yake kifuani mwa Magreth, ila hakuweza kupata nafasi ya kuyaona maziwa ya Magreth kama jinsi alivyo yaona akiwa ofisini kwake.
“Wiki ijayo nitasafiri kuelekea nchini Nigeria. Ninataka nikiondoka huku nyuma niwe nimesha kuachia mazingira mazuri kama nilivyo kuahidi mwanangu”
“Ohoo nitashukuru sana baba”
“Ila haya yote ambayo nitakufanyia. Tafadhali nina kuomba usiweze kumueleza mtu yoyote”
“Kwa nini baba?”
“Unajua mimi ni mtumishi wa Mungu. Endapo watu watatambua kwamba nimekufanyia haya yote. Wanaweza kuyapaleka mawazo yao mbali sana. Watazalisha skendo ambazo hakika sinto zipenda kwa maana watu hatuto wazuia kusema.”
“Baba ila sijakuelewa hapo kidogo?”
“Ni hivi endapo watatambua kwamba mimi nimekufungulia mgahawa, na kukupangishia nyumba. Watahisi kwamba mimi na wewe tuna mahusiano ya kimapenzi. Huoni hilo jambo lina weza kuleta mpasuko katika huduma ya kanisa langu?”
Magreth akakaa kimya huku akimtazama nabii Sanga usoni mwake.
“Ndio maana nahitaji usimueleze mtu yoyote. Haya yote nina fanya kwa kuguswa kwa matatizo yako. Nasiku zote ulikaa kimya ikiwa unapitia kipindi hichi kigumu”
“Nimekuelewa baba, sinto fungua kinywa changu kusema kwa mtu”
Nabii Sanga akamfikisha Magreth nyumbani kwake. Akavuta noti zenye thamani ya milioni moja kutoka kwenye kibunda cha pesa zake.
“Kalipe kodi ya siku hizi utakazo kaa kwenye hiyo nyumba. Kesho ununue simu ya maana ambayo tutakuwa tuna wasiliana sawa Mage”
Magreth macho yakamtoka. Kiwango hichi kikubwa chapesa hajawahi kukimiliki yeye binafsi. Leo kwa mara yake ya kwanza ana miliki kiwango hicho kikubwa cha pesa.
“Pokea tu mbona una shangaa”
“Mbona ni pesa nyingi baba?”
“Hakuna, unajua Mungu ana fungua baraka za mtu mmoja mmoja kwa aina yoyote aitakayo. Je unapenda kubaki kwenye umasikini kila siku, je unapenda kuishi kwenye maisha ya uswahilini kama hivi?”
“Hapana”
“Basi Mungu ana endelea kujibu maombi yako. Jambo la msingi usifanye jambo kinyume na mpango wa Mungu. Jitunze usichana wako hadi pale utakapo vishwa pete kanisani na mwanaume ambaye Mungu atakuwa amekuletea”
“Nashukuru sana baba Mungu akubariki”
Magreth alizungumza huku akichukua pesa hizo.
“Sinto weza kushuka na kuingia ndani. Acha niwahi nyumbani”
“Nashukuru sana baba mchungaji”
Magreth mara baada ya kuagana na mchungaji akashuka kwenye gari. Akasimama hadi nabii Sanga akatokomea na gari lake. Akapiga hatua na kupandisha ngazi za kibarazani, katika nyumba anayoishi. Akakutana na mama mwenye nyumba kwenye kordo.
“Leo umerudi mapema eheee?”
Bi Ngedera alizungumza kwa sauti iliyo jaa kejeli pamoja na dharau.
“Una nidai kiasi gani mama?”
“Thelathini na ninataka kodi yangu ya miezi sita”
“Hata ya mwaka ukihitaji nitakupa, ila hata hiyo miezi sinta sinto imaliza kwenye hii nyumba yako. Hivyo nakulipa deni lako la miezi miwili pamoja na mwezi huu.”
“Hiyo miezi iliyo baki vipi?”
“Hujanielewa kwamba sinto kaa kwenye hii nyumba yako. Mama una mdomo mchafu, tambua Mungu hapendi dharau kwa maana huwajui watu wapi wana tokea na wapi wataelekea”
Bi Ngedere akakosa la kuzungumza mara baada ya kuona Magreth akihesabu noti za shilingi elfu kumi kumi. Alipo ridhika ni kiwango gani anahitaji kumpatia bi Ngerede, akamkabidhi.
“Yaani wewe mama una bahati kwamba nina hofu ya Mungu. Ila kama ingekuwa si kuwa hivyo, leo ningekubamiza hadi ungenijua jina langu la utotoni nilikuwa naitwa nani”
Magerth alizungumza huku akifungua mlango wa ndani kwake na kuingia. Akamuacha bi Ngedere, akiwa amejawa na aibu kubwa.
                                                                                                                   ***
    Taratibu nabii Sanga akafunguliwa geti la kwanza kwenye jumba lake kubwa analo ishi na familia yake. Akafunguliwa geti la pili, na kusimamisha gari lake kwenye maegesho ya magari yake ya kifahari yapatayo kumi na tano. Msichana wa kazi, akawahi kusimama mlangoni mwa gari hilo kabla ya nabii Sanga kushuka.
“Shikamoo baba”
Binti huyo mwenye umri wa miaka kumi na tisa alisalimia kwa heshima kubwa akipokea koti la nabii Sanga.
“Marahaba. Mama yako yupo?”
“Hajarudi bado?”
“Hajarudi!! Amekwenda wapi?”
“Alitoka, mchana ila bado hajarejea”
“Haya kaweke koti langu ndani”
Nabii Sanga, akatoa simu yake mfukoni na kuitafuta namba ya mke wake. Akaipiga na kwa bahati mbaya akakuta haipatikani. Moja kwa moja akeleeka ndani, akamkuta mwanaye wa mwisho Julieth akijisomea.
“Shikamoo baba”
“Marahaba, vipi mbona una jisomea sebleni ikiwa maktaba kupo?”
“Ni kazi ndogo tu naimalizia”
“Mama yako alikuaga ana kwenda wapi?”
“Hakuniaga”
“Ulikuwepo alipo toka?”
“Hapana, nimerudi sijamkuta”
“Chuo vipi?”
“Safi tu dady. Alafu wiki ijayo tuna ziara ya kichuo kuelekea kwenye mbuga za wanyama ngorongoro. Itakuwa ni ziara ya siku tano”
“Kinatakiwa kiasi gani cha pesa?”
“Milioni mbili”
“Nitakupatia asubuhi”
Nabii Sanga akaelekea chumbani kwake. Akakitazama chumba hichi jinsi kilivyo pangwa vizuri kisha akavua nguo zake, akaingia bafuni, akaoga na kuvaa nguo nyingine. Akarudi sebeleni, akapata chakula cha usiku, huku saa ya ukutani ikionyesha ni saa sita kasoro usiku. Hadi binti yake pamoja na msichana wa kazi wanaingia kulala mke wake bado hajarejea kwenye safari ambayo hajafahamishwa.
‘Huyu mwanamke atakuwa amekwenda wapi?’
Nabii Sanga alizungumza huku akichukua simu yake na kupiga tena namba ya mke wake. Majibu aliyo yapokea awali ya kuto patikana kwa simu hiyo, ndio majibu aliyo yapokea muda huu. Akazima taa za sebleni na kukaa kwenye moja ya sofa huku giza likitawala eneo zima la sebleni. Baada ya nusu saa, akasikia, mngurumo wa gari la mke wake aina ya BMX X6. Hakunyanyuka kujisumbua kuwasha taa, akakaa kwenye sofa hilo ambalo mtu anaye ingia mlangoni anamuona vizuri. Mrs Sanga, akafungua mlango wa sebleni hapo taratibu huku akitembea kwa mwendo wa kunyata. Hakuwasha taa, ila kwa haraka nabii Sanga akawasha tv kubwa iliyopo sebleni hapa na kumfanya Mrs Sanga kustuka sana kwani hakutarajia kumuona mume wake akiwa eneo hilo.
“Unatoka wapi mke wangu?”
Nabii Sanga alizungumza huku akinyanyuka taratibu kwenye sofa hilo. Akaiweka rimoti mezani na kumsogelea mke wake aliye anza kutetemeka kwa woga.
“Saa saba kasoro ndio muda wa kurudi nyumbani?”
“Ahaa tulikuwa na huduma sehemu ya wamama, hivyo nilichelewa mume wangu. Nina kuomba unisamehe”
Nabii Sanga akawasha taa ya sebleni hapo na kumuona vizuri mke wake jinsi nywele zilivyo mtibuka.
“Naona mapepo walikuwa ni wagumu sana kutoka hadi nywele zimechanguka? Usiku mwema”
Nabii Sanga akapandisha gorofani na kumuacha mrs Sanga akijishika shika nywele zake na kushindwa kujua ni kwa nini alisahau kuziweka nywele zake sawa huko alipo toka.
                                                                                                              ***
    Asubuhi na mapema, Magreth akaandaa chai ya maziwa pamoja viazi vya kushemsha. Akaweka viazi hivyo kwenye hotpot kisha chai hiyo akaiweka kwenye chupa kubwa ya chai. Vitu hiyo akaviweka kwenye kikapu, alipo hakikisha kwamba kila jambo muhimu ambalo ana hisi kwamba Mgonjwa anaweza kula lipo tayari. Akajiandaa na kuianza safari ya kuelekea hospitali ya Mwanayamala. Kabla ya kufika hospitalini, akapita kwenye moja ya duka na kununua simu aina ya Tecno C9 ambayo siku zote amekuwa akiitamani na kuwaona baadhi ya marafiki zake wakiitumia na kuisifia.
Akasajili laini mpya, kutokana namba ya nabii Sanga ana ifahamu kichwani mwake, haikuwa shida kumpigia na kumfahamisha kwamba ana elekekea hospitalini na hiyo ndio namba atakayo itumia kuanzia leo.
“Sawa nikipata muda nitapitia hapo hospitalini”
“Sawa baba”
Magreth akafika hospitalini, akaulizia hali ya mgonjwa na kuelezwa kwamba alizunduka majira ya saa kumi usiku, ila kwa sasa ame lala.
“Amejitambua yeye ni nani?”
“Ndio na aliuliza kwamba yupo wapi? Nani amemleta na tukamjibu kila alicho kiuliza”
Nesi alimjibu Magreth huku akimtazama usoni mwake.
“Kwahiyo kuna matumaini ya yeye kupona?”
“Ndio”
“Nimemletea viazi vya kushemsha pamoja na chai ya maziwa je vitakuwa ni vyakula vizuri kwake?”
“Kwa viazi hapo ni sawa kidogo ila kwa chai hapana. Bado ana kidonda tumboni mwake”
“Ahaa sawa sawa”
Magreth akakaa hospitalini hapa hadi Evans alipo zinduka kutoka usingizi. Magreth akapewa nafasi ya kwenda kumuona tena katika wodi aliyo lazwa, kwani amehamishwa kutoka katika wodi ya wagonjwa mahututi hadi wodi ya wagonjwa wa kawaida na amepewa chumba cha kwake peke yake, hii ni kutokana na hadthi ya nabii Sanga.
“Hei wewe, hawajakudhuru wale wahuni?”
Evans alizungumza huku akitabasamu kwa furaha.
“Hapana, unajisikiaje?”
“Maumivu kwa mbali hapa tumboni”
“Pole sana rafiki yangu”
“Nashukuru kusikia hawajakudhuru. Washenzi wale nikitoka hospitalini nilazima niwawinde”
“Hapana usifanye hivyo. Unajua kwamba Mungu ana makusudi yake kwenye haya maisha yako. Munge amekupa nafasi nyingine ya kuishi, tafadhali usiizembee”
“Vyeti vyangu”
“Vyeti vyako, vipi tena?”
“Kwenye lile begi langu la mgongoni kuna vyeti vyangu vya kuanzia primary school hadi chuo kikuu”
Evan alizungumza huku akiwa amejawa na tahamaki kubwa sana. Magreth kwa kumbukumbu zake, akakumbuka wale vijana waliondoka na mabegi yote mawili. Kabla hajamueleza chochote, mlango ukafunguliwa ana akingia nabii Sanga.
“Kijana amepata nafuu?”
“Karibu baba”
“Nashukuru Mage”
“Kaka huyu ni baba yangu wa kiroho anaitwa nabii Sanga”
“Jina na sura sio ngeni kwangu, nilisha wahi kukuona kwenye kitoa cha tv ukihubiri?”
“Ndio hujakosea kabisa. Ninaona maombi niliyo yafanya yameleta bamadiiko na kuzaa matumaini mapya. Unaitwa nani kijana?”
“Evans Shika”
“Nashukuru kukufahamu. Nilipita hapa mara moja, ila kuna kikao cha wachungaji mahala fulani, inabidi niende. Ila Magreth nakuomba tuzungumze nje mara moja”
“Sawa baba”
Nabii Sanga akaaga, kisha wakatoka katika chumba hicho alicho lazwa Evans na kusimama kwenye kordo.
“Sehemu ya kufungua mgahawa imepatikana pia nyumba imepatikana, hivyo nikiwahi kutoka kwenye mkutano nitakupitia twende ukazione hizo sehemu, kama utazipenda basi tutazichukua, ila kama utakuwa hujazipenda, basi tutatafuta nyingine”
Habari hiyo ikamuacha Magerth mdomo wazi, macho yakamtoka huku akijaribu kuzuia mlipuko wa furaha yake. Nabii Sanga akatoa laki mbili na kumkabidhi Magreth bila ya kumuambia ni za nini hizo pesa. Akaondoka huku simu yake akiweka sikioni, akizungumza na mmoja wa wachungaji katika kanisa lake. Magreth akatamani kumfwata ila akashindwa, akazitazama pesa hizo na kuzishika vizuri, kisha akarudi ndani ya chumba hicho.     Magreth na Evans, wakajikuta wamezoeana kwa muda mfupi sana huku kila mmoja akimuelezea mwezake maisha ya nyuma. Japo wote wametoka kwenye maisha ya kimasikini, ila kidogo maisha aliyo yapitia Evans yana mateso makubwa sana kuliko maisha ya Magreth.
Majira ya jioni, nabii Sanga akampitia Magreth hospitalini hapo na moja kwa moja wakaelekea maeneo ya Kinondoni, wakapelekwa na Tomas kwenye eneo la mgahawa, hakina ni eneo zuri sana na kuna mzunguko mkubwa wa watu.
“Nyumba ipo mbali na hapa?”
“Hapana baba mchungaji, ipo hapo mtaa wa nyuma”
Wakaelekea eneo la nyumba, wakasimama kwenye nyumba ya gorofa moja.
“Ndio hapa baba mchungaji, tunaweza kuingia ndani?”
Wakaingia ndani ya nyumba hii nzuri, ambayo muda wote imemuacha Magreth mdomo wazi.
“Wamesema ni kiasi gani?”
“Milioni mia sita hamsini, ila nimezungumza nao, hadi kwenye milioni miatano watauza”
“Mage umeipenda hii nyumba”
“Ndio baba ila mbona kodi yao ni garama kiasi hicho?”
“Hapana, jana usiku nilibadilisha mawazo, nikaona nisichukue nyumba ya kupangisha ila ninunue kabisa. Nina imani utaishi kwa amani kabisa kwenye hii nyumba”
Maneno ya nabii Sanga kidogo, yakabakisha kidogo yamuangushe Magreth kwa furaha. Katika maisha yake hakutarajia hata siku moja kuja kumiliki nyumba ya kwake peke yake, tena nyumba yenye hathi ya mamilioni ya pesa.
                                                                                                   ITAENDELEA
Nabii Sanga anaendelea kufanya maajabu kwenye maisha ya Magreth .Je kwakufanya hivyo atafanikiwa kupata bikra ya Magreth anayo itamani kupita kitu chochote kwenye maisha yake?  Endelea kufAatilia kisa hiKIi cha kusisimua, usikose sehemu ya 04

 


from MPEKUZI

Comments