Polisi Aliyemuua Kikatili Mmarekani Mweusi Ashitakiwa kwa Mauaji ya Bila Kukusudia

Afisa wa polisi anaetuhumiwa kwa mauaji ya kikatili ya  Mmarekani mweusi, George Floyd ametiwa mbaroni na kushtakiwa kwa kosa la mauaji   kufuatia kifo cha Raia huyo mweusi ambaye alimuua kwa kumkanyaga shingo na kumfanya akose pumzi

Hayo yanatokea katika kipindi ambacho mamlaka nchini  humo zimetangaza marufuku za kutotoka nje baada ya vurugu za maandamano ya siku tatu ambazo zimesababisha baadhi ya maeneo kuchomwa moto. 

Derek Chauvin, afisa wa polisi mzungu ambae alichukuliwa video, ikionesha kambana kwa kutumia goti shingoni, marehemu George Floyd kwa karibu dakika tisa, anashitakiwa kwa kusababisha kifo pasipo kukusudia


from MPEKUZI

Comments